Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa kuna Ongezeko kubwa la Wawekezaji katika Sekta ya Utalii hatua inayochangia Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya nchi.
Amebainisha kuwa Ongezeko hilo la.Wawekezaji pia linachangia Ongezeko la Watalii wanaotembelea nchini hali inayoiimarisha sekta ya Utalii.
Rais Dk, Mwinyi ametoa Tamko hilo alipoweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hoteli ya SSPD-BUHAIRAN iliyopo Bwejuu Mkoa Kusini Unguja Inayomilikiwa na Wawekezaji kutoka Falme za Kiarabu.
Rais Dk, Mwinyi amefahamisha Kuwa Faida za Utalii ni Kubwa kwa nchi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kuwahimiza Wananchi kuendelea Kuwaunga Mkono Wawekezaji wanaowekeza maeneo mbalimbali.
Amezitaja Faida hizo kuwa ni pamoja na Fursa za Ajira kwa Vijana zile moja kwa moja na nyengine zisizo za moja kwa moja , Upatikanaji wa soÄ·o kwa bidhaa zinazozalishwa na Wakulima na Wavuvi kwa bidhaa za Baharini na Ongezeko la Pato la Taifa.
Akizungumzia Uwekezaji wa Hotel hiyo aliyoielezea kuwa ya Viwango Rais Dk,Mwinyi ameeleza kufunguliwa kwake kutafungua Milango kwa Zanzibar kupokea Wageni wengi zaidi kutoka Falme za Kiarabu.
Aidha amewapongeza Wananchi wa Bwejuu na Mkoa wa Kusini kwa Kuonesha Utayari wao na Kuwakaribisha Wawekezaji hao.
Wakati huohuo Rais Dk Mwinyi ameridhia Ombi lililowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhammed Mahmoud kwa niaba ya Wananchi la kutengenezewa Barabara Ya Kilomita Tatu kwa Kiwango cha lami Kutoka Michamvi Mashariki hadi Michamvi Magharibi.
Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Mmiliki na Muekezaji wa Mradi huo Dk, Muhammed Omar ameishukuru Serikali kwa kukubaliwa kuwekeza Mradi huo aliouelezea kuwa Utawanufaisha Wakaazi wa eneo hilo kwa Fursa za ajira 500 pamoja na kuchangia Uchumi wa nchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar ( ZIPA) Saleh Saad Muhammed amefahamisha kuwa katika Kipindi cha Miaka minne ya Awamu ya nane ZIPA imesajili zaidi ya Miradi ya Uwekezaji 430 ikiwa na thamani ya takriban Shillingi Bilioni 5.6 itakayotoa fursa za ajira 25,000.
Ufunguzi wa Mradi huo ni miongoni mwa Shamrashamra za Sherehe za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanziibar.
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19