Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Chunya
SHULE ya Msingi Matwiga iliyopo wilayani Chunya mkoani Mbeya imepatiwa msaada wa Madawati 41, ambayo yatasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa Madawati na hivyo kupelekea kiwango cha elimu kupanda kwa wanafunzi kutokana na uwepo wa madawati ya kutosha tofauti na ilivyokuwa awali .
Madawati hayo yamekabidhiwa Mei 19,2025 na Diwani wa viti maalum kata ya Matwiga,Neema Mwakaniemba kwa kushirikiana na mwanae aitwaye Lusajo Mwakibibi.
Diwani huyo amesema kuwa Kwa kushirikiana na mtoto wake wamekabidhi Madawati 41 Shule ya Msingi Matwiga iliyopo kata ya Matwiga Halmashauri ya wilaya ya Chunya, kwa lengo la kusaidia wanafunzi katika zoezi la ujifunzaji na ufundishaji jambo ambalo litaleta hamasa ya kusoma bidii kwa wanafunzi wa Shule hiyo.
Wakizungumza wakiwa katika viwanja vya shule ya msingi Matwiga Mama na mtoto wamesema maono ya kutoa madawati hayo yametokana na namna walivyoshirikishwa uhaba wa madawati shuleni hapo lakini moyo wa kutoa ulikuwa ndani yao na msukumo mkubwa wa kutengeneza madawati hayo.
“Wazo la kutoa dawati hizi lilitoka kwa mwanangu na mimi niliamua kumuunga mkono kwa kutengeneza dawati 10 wakati yeye ametengeneza dawati 31 hivyo kufanya jumla ya madawati kufika 41 “amesema Diwani huyo .
Aidha aliwaomba wanawake pamoja na vijana kukumbuka kwao kwa kutumia mali au fedha ambazo Mungu amewapatia katika kuendeleza maeneo yao.
“Kupata wazo ni jambo moja lakini kuchukua hatua ni jambo lingine, nilipopata wazo la kuleta dawati hapa shuleni nilimshirikisha Mama yangu lakini nilimhirikisha Mke wangu wote walinielewa ndipo nikaanza kutengeneza dawati hizi “amesema “amesema Lusajo Mwakibibi.
Hata hivyo amesema kuwa jambo kubwa aliloweza kufikiri ni watu gani na nitawasaidia ndicho kilichomsukuma kufanya huku alisema kutaja gharama aliyotumia katika utengenezaji wa Madawati hayo si muhimu kwake.
Diwani wa kata ya Matwiga, Frank Malambughi amemshukuru Mhe Neema Mwakaniemba (Diwani viti maalumu Halmashauri ya wilaya ya Chunya kutokea kata ya Matwiga) pamoja na mwanaye kwa msaada wa madwati hayo huku akiwasisitiza wananchi wa Matwiga na hata wananchi wa Tanzania kwa ujumla kutumia tukio hilo kama Mfano bora na wa kuigwa
Naye Afisa Elimu kata ya Matwiga Mwalimu Monica Kulanga amesema tendo la kutoa madawati hayo kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Matwiga ni la Kiroho maana Malaika wa Mungu (Wanafunzi) wa kila hali wakiwepo yatima na wanafunzi mbalimbali watatumia kukalia wawapo darasani.
Mwalim Mkuu wa Shule ya Msingi Matwiga mwalimu Godfrey Kikoti ameshukuru sana wadau kutoa madawati hayo kwa Shule yake, akiongeza kuwa yatasaidia sana kupunguza wanafunzi kukaa wengi kwenye dawati moja jambo ambalo haliwavutii wanafunzi kupenda shule lakini uwepo wa madawati haya kutaongeza motisha kwa wanafunzi ya kusoma, motisha ya kufundisha kwa walimu pia itaongezeka
Madawati hayo yametolewa na Neema Mwakaniemba Diwani wa Viti maalumu Halmashauri ya wilaya ya Chunya pamoja na mtoto wake Ndugu Lusajo Mwakibibi na yamepokelwa na mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Matwiga huku Diwani wa Kata ya Matwiga Mhe Frank Malambughi na viongozi wengine wa Chama na Serikali wakishuhudia makabidhiano hayo.

More Stories
Dkt.Biteko mgeni rasmi maadhimisho miaka 35 ya TAWLA
TDB yaonya wanaonunua maziwa kwenye chupa za plastiki
Dkt.Ndumbaro:Rais Samia ameweka historia kufanya Urekebu wa sheria kwa kutumia fedha na wataalamu wa ndani