Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
DIWANI wa Kata ya Kimara Eng. Ismail Mvungi leo Aprili 7, 2024, ameshiriki katika mashindano ya Quran yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Paradigms uliopo Kata ya Kimara Wilayani Ubungo.
Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Maarifa Islamic Foundation, chini ya Mkurugenzi wake Sheikh. Waziri Zambiko huku Diwani wa Kata hiyo akiwa mgeni rasmi.
Mara baada ya mashindano hayo, Mkurugenzi wa Maarifa Islamic Foundation, amemkabidhi cheti Cha pongezi Diwani Mvungi ikiwa ni kutambua mchango Mkubwa wa kuwezesha mashindano hayo ya Quran.
Lakini pia, uongozi Bora ndani ya Kata ya Kimara, kutokana na Diwani huyo kushiriki kwa ukaribu zaidi shughuli za kijamii na kidini ndani ya Kata yake.
Akizungumza mara baada ya mashindano hayo, Diwani Mvungi amewapongeza wale wote walioshiriki huku akiwasifu kutokana na kuonesha vipaji vya hali ya juu katika kuhifadhi Quran.
Vilevile, ameipongeza Taasisi ya Maarifa Islamic Foundation kwa kuandaa mashindano hayo na kuahidi kuwa bega kwa bega kuhakikisha taasisi hiyo inatanua wigo.
Eng. Mvungi amekabidhi zawadi kwa washindi wote wa Quran walioshinda katika mashindano hayo.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa