December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Kimji aeleza Mafanikio ya Rais Samia Ilala

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Diwani kata ya Ilala Saady Kimji ,amesema wanajivunia Mafanikio makubwa Rais Samia amewapatia miradi mikubwa ya maendeleo katika uongozi wake ambapo miaka mitatu ya Dkt.Samia Suluhu Hassan wameweza kupata Barabara za kisasa ,vituo vya afya na shule za kisasa.

Diwani Saady Kimji alisema hayo wakati wa Uzinduzi wa Kisima cha maji safi na Salama mtaa wa Mafuriko Ilala Bungoni kilichoxinduliwa na Waziri wa Maji Juma Aweso.

“ILALA tunajivunia Mafanikio makubwa ya Serikali ya Dkt samia suluhu Hassan kata ya Ilala tumepokea fedha nyingi za miradi ya maendeleo awali ikiwemo sekta ya afya na elimu na miundombinu ya Barabara zimejengwa na zinaendelea kujengwa na zingine zimekamilika ambapo barabara za lami kilometa 4 “alisema Kimji

Diwani Saady Kimji alisema katika mtaa huo pia Serikali imejenga Zahanati ya kisasa ni jitihada za Rais na Mbunge kupitia pesa za wadau ambapo kwa sasa imekamilika pamoja na miundombinu yake.

Aidha alisema pia pesa za Mana zinefanikisha kujenga shule ya kisasa Ilala ya Mchepuo wa kingereza English Medium kwa sasa imeshaanza kutoa huduma shule ya MZIZIMA.

Pia Rais Dkt Samia ametoa shikingi milioni 60 ya ofisi ya Serikali za mitaa na pesa za shule ya sekondari ya golofa Msimbazi na Gholofa nne ya shule ya Sekondari Mussa Azzan Zungu.

Katika hatua nyingine alisema kura zote za Ilala ziende kwa Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu kwa utekelezaji wa Ilani vizuri wananchi wote watapiga kura mwaka 2025