December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Johari awataka wazazi kufundisha watoto maadili

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

DIWANI wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Asha Johari ,amewataka Wazazi wa kusimamia maadili kwa watoto na kukemea vitendo vya ukatili.

Diwani Asha Johari ,ameyasema hayo katika mahafali ya 59 Darasa la saba shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko wilayani Ilala.

” Wazazi wezangu wa wanafunzi hawa wanao hitimu leo elimu ya msingi nawaomba muwafundishe watoto maadili mema ili wawe kioo cha jamii na kuwa mabalozi wazuri huko wanapoenda “amesema Johari

Diwani Johari, amesema kumaliza elimu ya msingi sio mwisho wa elimu ni mwanzo watakapofundishwa maadili mema watakuwa mabalozi wazuri Taifa letu litapata kizazi chenye maadili mema.

Amewataka Wazazi kwenda kuwaanda watoto kwa ajili ya kidato cha kwanza wakajisomea wakisubiri matokeo yao wasiwaache wakaingia katika makundi hatarishi.

Amepongeza uongozi wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko kwa matokeo yao kila mwaka inaendelea kufanya vizuri katika matokeo yake ya ufaulu..

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko Sezaria Kiwango ,amesema mahafali ya 59 ya shule hiyo wahitimu mwaka huu 69 shule hiyo imetimiza miaka 102 ilianzishwa mwaka 1964 .