December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Johari awataka Wazazi Ilala kulea watoto kwa misingi bora

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Diwani wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Asha Johari,amewataka Wazazi Ilala kulea watoto kwa misingi Bora ili waweze kuwa na maadili mazuri wasiingie katika mmomonyoko wa maadili.

Diwani Asha Johari alisema hayo katika Mahafari ya Darasa la saba shule ya Msingi uhuru Mchanganyiko ambapo wanafunzi 85 katika Mahafari 58 walihitimu elimu ya msingi katika shule hiyo na kupewa vyeti. .

“Nawaomba Wazazi wangu wa Ilala tuwalehe watoto wetu katika misingi bora ili waweze kufanya vizuri kitaaluma darasani waweze kufaulu wasiingie katika mmomonyoko wa maadili “alisema Johari.

Diwani Asha Johari, alisema Dunia kwa sasa Imebadirika kutokana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili hivyo aliwataka Wazazi kushirikiana na Walimu ili wanafunzi wao waweze kufanya vizuri na kukuza taaluma shuleni katika kuongeza ufaulu.

Aliwataka wahitimu hao wa darasa la saba wa shule hiyo wawe mabalozi wazuri huko wanapoenda wakatangaze shule hiyo ambayo inafanya vizuri kila mwaka wanafunzi wanafaulu asilimia 100 kila mwaka.

Aidha aliwataka Wazazi wa wanafunzi wanaohitimu katika shule hiyo kuwasimamia watoto wao Wasiende katika makundi badala yake waendelee kujisomea wakati wakisubiri matokeo yao ya kwenda kidato cha kwanza.

Mwalimu mkuu wa shule ya Uhuru Mchanganyiko Selaria Kiwango alisema. Shule uilianzishwa mwaka 1921 ikiitwa Goverment Afrika Sekondari school Dar es Salaam mwaka 1953 ilihamishiwa Morogoro ikaitwa Kichwele Afrikan Boys middle School ikiwa na darasa tano mpaka darasa la nane.

Mwaka 1962 ilianzisha kitengo cha wanafunzi wasiiona mwaka 1964 shule hiyo ilibadilishwa jina na kuitwa shule ya Msingi UHURU MCHANGANYIKO ikiwa na darasa la kwanza mpaka la saba ikiwa chini ya Serikali Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.

Diwani wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Asha Johari akikabidhi vyeti kwa Wahitimu wa darasa la saba Shule ya Msingi uhuru Mchanganyiko wilayani Ilala leo October 06/2023 (HERI SHAABAN )
Diwani wa Viti Maalum Asha Johari akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba waliohitimu elimu ya msingi shule ya msingi uhuru Mchanganyiko katika Mahafari ya 58 jumla ya wanafunzi 85 walipewa vyeti (Picha na Heri Shaaban)
Wahitimu wa darasa la saba shule ya Msingi uhuru Mchanganyiko wilayani Ilala wakiwa katika Mahafali yao leo October 06/2023 Mgeni rasmi Diwani wa viti Maalum wilaya ya Ilala Asha Johari (Heri Shaaban