Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Diwani wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Magreth Cheka, amewataka waumini wa Kanisa la Anglikana Dayosisi Mtakatifu Aidano Karakata Kipawa kuendeleza Amani ya nchi yetu na kufanya ibada
Diwani Magreth Cheka, alisema hayo wakati wa harambee maalum ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dar es Salaam Mtaa mtaa Mt,Aidano Karakata Kipawa wilayani Ilala,ambapo Diwani Cheka alikusanya shilingi milioni 3.3 katika kanisa hilo zilizochangwa na Waumini .
“Mimi ni muumini wa Kanisa la Katoliki leo nimeshiriki ibada maalum ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hili la Anglikana nimeshiriki ibada na waumini mimi Diwani wenu nawaasa tuendeleze Ibada na kuomba Amani ya nchi yetu alisema Cheka .
Diwani Cheka aliwataka waumini kujenga umoja na kushirikiana pamoja katika kuleta maendeleo na kufanya ibada tulinde tunu yetu tulioachiwa na waasisi wetu Mwalimu Julius Nyerere.
Katika harambee hiyo Diwani cheka na Diwani wa Kipawa Aidan Kwezi walichangia shilingi 500,000 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Kanisa .
Akizungumza katika Harambee hiyo Kasisi wa Kanisa hilo Gerikoshua Gidio Baliko alisema harambee hiyo wanakusudia kukusanya shilingi milioni 40 wanaendelea kukusanya mpaka mwezi Desemba.
Kasisi Baliko alisema katika uzinduzi huo wamefanikiwa kukusanya shilingi milioni 3.3 ambapo cash zilipatikana shilingi 2,602000/= zilizoingizwa katika akaunti ya Kanisa shilingi 660,000/=njia ya simu 70000/=zilizokusanywa siku ya nyuma 3,025,000/=jumla kuu 6,357,000/=.
Aliwataka waumini wa Anglikana na wadau mbalimbali kuendeleza michango ili malengo ya ujenzi yaweze kutimia.
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito