Na Heri Shaaban , TimesMajira Online, Ilala
Diwani wa Viti Maalum wilaya ya Ilala mwl Beatrice Edward , kutoa msaada wa haraka wa kunyonya maji taka katika kituo cha Mwana Islamic Fondation kilichopo Vingunguti Wilayani Ilala walichokitembelea hivi karibuni kukuta changamoto.
Wakati wa kutoa msaada huo Diwani mwl, Beatrice Edward, ameongozana na Madiwani wa Temeke wa Viti Maalum Mariam Mtemvu na Viti Maalum Kinondoni Diwani wa Josephine Wage, Katibu UWT Kata ya Vingunguti na uongozi tawi UWT walifika kituo cha Mwana Islamic kutoa msaada wa kuvuta maji taka katika kituo hicho kwa msaada wa udhamini wa ADOLPH NYAGABONA MAKAYA ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la DIASPORA Tanzania , DUNIANI es( TDC) GLOBAL
Mimi na Madiwani wezangu wa Viti Maalum kutoka Temeke Mariam Mtemvu na Diwani wa Viti Maalum Kinondoni mama Wage tumefanya ziara katika kituo cha Mwana Islamic Fondation kutatua changamoto Mbalimbali leo kero imetatuliwa alisema mwl ,BEATRICE
Diwani Mwl, Beatrice Edward ,alimtaka Mlezi wa kituo cha Mwana Islamic Fondation kulea Watoto wa kituo hicho katika Mazingira mema chama cha Mapinduzi kipo pamoja nao katika kutatua changamoto zao .
Mlezi wa kituo cha Mwana Islamic Fondation Saada Omary, Mama Mwana alisema kituo cha Mwana Islamic Fondation kina watoto 65 wanawake 30 na wanaume wapo 35 wengine wanasoma shule ya Msingi na shule ya awali kituo kilianzishwa mwaka 2005 awali kikiwa na watoto saba kinapokea pia watoto wanaoletwa na Serikali wakiwemo watoto wachanga .
Diwani wa Viti Maalum wilaya ya Temeke Mariam Mtemvu, alitoa wito kwa Wadau kujitokeza katika kusaidia makundi maalum waweze kujiendesha .
Mwakilishi wa Watanzania nje DISPORA Patricia Nyamis, alisema kilichomgusa kutoa msaada huo baada kupewa taarifa na Diwani wa wilaya ya Ilala Beatries Edward, kutokana na changamoto za Kituo hicho ambapo alisema DISPORA watasaidia kituo hicho kwa kushirikiana na Diwani Beatries .
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi