January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Beatrice atoa mkono wa Pasaka

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Diwani wa Viti Maalum Wilayani Ilala Mwl, Beatrice Edward, ametoa mkono wa Pasaka kwa Watoto wa Makundi Maalum , wa Kituo cha Mwana Islamic Fondation .

Akikabidhi msaada huo Diwani Beatrice alisema watoto wa Makundi Maalum sawa na watoto wengine wanaitaji kupewa faraja na jamii .

” Leo naungana na Katibu wa Mkuu wa DIASPORA Tanzania (TDC) GLOBAL kupeleka sadaka kwa ajili ya sikukuu hii ya Pasaka katika kituo cha Mwana Islamic Fondation” alisema Mwl , Beatrice .

Mwalimu Beatrice alisema misaada hiyo ya CHAKULA waliotoa katika kituo hicho ni mchele,maharage,Tambi,Mkaa ,nyanya ,Vitunguu ,maziwa ya watoto Lactogen ,karoti ,hoho,na mafuta ya kula .

Aliwashukuru wadau mbalimbali ambao wanamshika mkono kwa ajili ya kituo hicho cha Watoto wa Makundi Maalum kutatua kero mbalimbali .

Aliwataka Wananchi kujenga tabia ya kutembelea katika makundi maalum kula nao chakula au kuwafatiji kwani wao sawa na watu wengine ambao wanaitaji faraja katika Jamii .