January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Banigwa agawa Baskeli kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

DIWANI wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Dkt.Julieth Banigwa, amewagawa Baskeli kwa Wanafunzi wawili wenye Ulemavu ili waweze kwenda shule kusoma .

Dkt.Julieth Banigwa, aligawa Baskeli hizo za miguu miwili katika mkutano wa Wajasiriamali Wanawake ulioandaliwa na Diwani Banigwa kwa ajili ya kuwapa elimu ya mikopo na kuelezea masuala ya ukatili na maadili kwa jamii.

“Nimeguswa hawa watoto wawili walikuwa wana changamoto ya ulemavu nimewapatia Baskeli ili wawe wanaenda shule leo nimefanikisha kuwapa baskeli hizi za miguu miwili waweze kuzitumia nyakati kwenda shule kusoma “alisema Dkt.Banigwa.

Dkt.Julieth Banigwa alisema anaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan sera ya Elimu bila malipo leo amevutika kuwasaidia Wanafunzi hao wawili wenye mahitaji maalum waweze kusoma.

Aidha aliwataka wadau wengine kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusaidia jamii yenye makundi maalum misaada mbali mbali ya kijamii.

Katika hatua nyingine aliwataka wanawake kuhitatumbua katika kusimamia watoto waweze kupata haki ya msingi waweze kusoma na kukomesha vitendo vya ukatili .

Alisema mtoto wa mwezako ni wako hivyo tushirikiane na Serikali katika kukemea vitendo vya ukatili kila mmoja awe mlinzi wa kulinda mtoto wa mwezake .

Aliwataka Wazazi kuwafichua watoto wenye ulemavu watambulike ili waweze kupata elimu kwani ni haki yao ukiwaweka ndani watakosa haki zao za msingi ikiwemo elimu .

Afisa Ustawi wa Jamii wa kata ya Segerea Malisela Olwa alizungumzia ukatili na malezi kwa watoto akiwataka Wazazi wakumbuke wajibu wao katika malezi ya watoto kwa ujumla ambapo ikitokea changamoto za ukatili wa kijinsia waweze kutoa taarifa na kuitaka jamii kuwa macho.