Na Heri Shaaban, Timesmajira Online, Ilala
DIWANI wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Aisha Johari, ametoa kadi za Bima ya Afya kwa watoto wa mahitaji maalum Kata ya Liwiti wilayani humo.
Akikabidhi kadi hizo pamoja na viongozi wa UWT Kata ya Liwiti,Johari, amewataka wazazi wa watoto hao kuzitumia bima hizo katika vituo vya afya vya Serikali .
Pia amesema anaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia jamii upande wa sekta ya afya kwa watoto hao kupata matibabu.
Aidha amewahimiza wananchi kusaidia watoto wa makundi maalum katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu na afya.
Katibu wa UWT Liwiti, Habiba Rajabu,amemshukuru Diwani huyo kwa kuwakumbuka watoto hao katika suala Zima la afya
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Misewe Kata ya Liwiti Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam Said Matossa, amesema katika mtaa wake kuna watoto wa mahitaji maalum zaidi 15,hivyo amewahimiza Madiwani wengine na wananchi, kuweka utaratibu wa kutembelea watoto wa makundi maalum kwa ajili ya kuwasaidia.
More Stories
Rais Mwinyi:Tuzindue mpango wa ujuzi kwa vijana katika uchumi wa buluu
Dkt.Mpango ashiriki dua,kumbukizi miaka 53 ya Hayati Karume
Wasira:Ilala kuna watu wameanza kampeni