December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani awafungulia fursa za ajira vijana

Na Irene Clemence, Timesmajira Online Dsm

KATIKA kukabiliana na changamoto ya vijana kukosa ajira, Diwani wa Kata ya Mzimumi Manispaa ya Kinondoni, Manfred Lyoto ameanzisha mkakati wa kuwatafutia kazi vijana katika makampuni sambamba na kuwaanzishia miradi ili kupunguza tatizo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Lyoto, amesema vijana ni nguvu kazi ya taifa hivyo kupitia ajira na miradi wataweza kujikwamua kiuchumi.

“Kupitia mkakati huu ambao nimeuanzisha na imani nitaweza kuwakwamua vijana katika kata yangu ya Mzimuni na hatimaye waweze kujitegemea wenyewe na kutegeneza kipato chao ,” amesema Lyoto.

Amesema kwa sasa vijana wengi wamekata tamaa ya maisha na kusababisha wengi wao kujikita katika masuala ambayo hayana msingi kwao na kwa taifa kwa ujumla .

“Katika Kata ya Mzimuni, tayari nimefanikiwa kuwatafutia ajira vijana 60 katika kampuni mbalimbali kati yao, vijana 35 wamekuwa wakishidwa kuendelea na kazi na kusababisha kufukuzwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukata tamaa,”alisema Lyoto.

Amesema kuwa kutokana na chagamoto ya vijana wengi waotafutiwa kazi kuacha , Diwani huyo amekuwa na utaratibu wa kuwapatia elimu juu ya masuala ya kazi kama njia ya kuwajenga kiakili ili waweze kujitambua na kuwa makini katika kazi zao.

Aidha aliwataka vijana katika Kata hiyo wanapopata nafasi hizo za kazi kutozichezea na badala yake wajitume na kufanya kwa bidii kwasababu taifa linawategemea wao.

Pia amewaomba viongozi wa dini kutoa elimu kwa vijana juu ya masuala mazima ya maadili ili waweze kujitambua wao ninani katika jamii.

” Sisi kama wanasiasa tunayonafasi katika kuwaelimisha vijana lakini peke yetu atuwezi nawaomba viongozi wa dini nao waendelee kutoa elimu juu maadili kwani ndio msingi katika maisha ya Sasa,”amesema Lyoto.

Hata hivyo amewaomba wananchi wa Kata hiyo kuendelea kumuunga mkono katika masuala mbalimbali anayoyafanya katika kata hiyo na kuwaomba wajitokezd kwa wingi pindi anapoitisha mikutano ya hadhara.