October 1, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Asha awafunda wanafunzi wa kike

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

DIWANI wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Asha Johari, amewataka wanafunzi wa Shule za Msingi Uhuru Mchanganyiko wenye Mahitaji maalum wasikubali kuchezewa katika miili yao badala yake amewataka wanafunzi wazingatie masomo .kila wakati.

Diwani Asha Johari alisema hayo katika shule hiyo jana wakati wa kukabidhi Mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi wa shule hiyo ikiwemo Sabuni wakati walipoenda kuzungumza nao na kuwapa semina kuhusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Watoto wangu kuna vitendo vya ukatili wa kijinsia wanafanyiwa watoto nawaomba msikubali mchezewe miili yenu kunapotokea vitendo hivyo mtoe taarifa haraka ili waweze kukamatwa wachukuliwe na vyombo vya sheria” alisema Asha.

Diwani Asha alisema kuwa kuna vitendo vya kishetani ambavyo avimpendezi Mwenyezi Mungu masuala ya ubakaji hivyo aliwataka jamii kuungana na kukemea vitendo hivyo mara moja .

Aidha aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo badala yake wasikubali kupigwa na kudanganywa au kunyanyaswa au kutumika kama kuna jambo tofauti watoe taarifa kwa Walimu au kwa Wazazi wao.

Alisema Dunia ya sasa imekuwa kijiji wana uwezo wa kufanya jambo lolote hivyo wasijione wanyonge wala kubaguliwa wao sawa na jamii nyingine .

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi ambapo katika jimbo la Ilala Rais Samia kwa kushirikiana na Mbunge wetu Musa Zungu ametekeleza miradi ya sekta ya Elimu kwa kujenga shule nyingi na sekta ya afya na miundombinu ya Barabara sasa hivi jimbo la Ilala Barabara zote zimewekwa lami na zinaendelea kuwekwa lami.

Katibu wa Wazazi kata ya Gerezani Jamila Simba aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo yao ili waweze kufanya vizuri kitaaluma Darasani na katika mitihani yao mbali mbali.