Judith Ferdinand, Timesmajira Online,Mwanza
Katika kipindi cha miaka minne jumla ya miradi 45 yenye thamani ya bilioni 2.6, imetekeleza Kata ya Kayenze wilayani Ilemela mkoani Mwanza,huku mingine ikiendelea na utekelezaji.
Hayo yameelezwa na Diwani wa Kata ya Kayenze Issa Mwalukila,wakati akizungumza na Timesmajira Online mara baada ya kufanya ziara Kisiwa cha Bezi,ambacho ni moja ya mtaa unaounda Kata hiyo.

Mwalukila, amesema,kwa upande wa Mtaa wa Kisiwa cha Bezi,mambo yamefanyika mengine ambapo wakati anaingia kwenye Udiwani mwaka 2020,shule ya msingi Bezi ilikuwa na madarasa matatu sasa yapo ya kutosha,nyumba ya walimu ambao umekamilika na wanaishi walimu wawili.
Lakini bajeti ya mwaka huu shule hiyo imepangiwa milioni 30, kwa ajili ya kuongeza nyumba nyingine ya walimu,huku katika eneo hilo pia wamewezeshwa huduma ya mawasiliano kwa kujengewa mnara kisiwani hapo.
Pia Kisiwani humo katika bajeti ya mwaka huu watapata barabara yenye urefu wa Kilomita 2,ambayo itajengwa kwa mawe.
Amesema,pia Kisiwa hicho kinapata zahanati ambayo wakati anaingia mwaka 2020 alikuta ipo katika hatua ya msingi ambao ulikuwa umejengwa na wananchi.
“Nilipeleka mahitaji ya wananchi wa Mtaa wa Bezi serikalini,ambapo tumepatiwa jumla ya milioni 202, kati ya hizo milioni 101 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo ambayo kwa sasa imefikia hatua ya boma na million 101ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya,ambapo wananchi wameshiriki katika ujunzi wa zahanati hiyo,”amesema Mwalukila.
Ambapo ameeleza kuwa wananchi wa Kisiwa cha Bezi walikuwa wanakabiliwa na changamoto hasa kwenye kipindi cha mlipuko wa magonjwa wamepotezwa ndugu kwa sababu ya kukosa huduma za afya.
“Kwani mpaka muda wa kutafuta mtumbwi kwa ajili ya kuwavushwa kwenda Kata ya Sangabuye kwenye kituo cha afya ilikuwa inachukua muda mrefu na asilimia kubwa walikuwa wanapotezwa maisha,wajawazito ilikuwa changamoto wakati mwingine ikikaribia miezi ya kujifungua ilimlazimu kuvuka maji kwenda kupanga ilikuwa karibu na huduma hivyo kuongeza gharama za maisha,lakini jibu sahihi linaenda kupatikana hivyo huduma za afya zinaenda kupatikana na watu wa Bezi wanaenda kuishi salama,”.

Ambapo ameeleza kuwa hayo yote yamefanyika kwa ushirikiano wa Serikali, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula,yeye Diwani na Wananchi ambao wamewekwa nguvu zao kwa wamesomba tofali na kazi nyingine.
Pia amesema,katika miaka yake ya uongozi anajivunia mambo mengi sana, ikiwemo kuwaunganishia wananchi huduma,kushiriki kwenye miradi kwa kushirikiana na wananchi, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Shule ya sekondari Kayenze wakati anaingia madarakani kulikuwa na madarasa 4 lakini sasa yameongezeka zaidi ya 11,shule ya msingi Chasubi kulikuwa na madarasa 7 sasa yapo 12.
Aidha shule ya msingi Chasubi matundu ya vyoo 16,awali ambayo hayakuwepo,milioni 500 walipewa kwa ajili ya huduma za afya.
“Serikali ikatuongezea milioni 300 kwa ajili ya vifaa tiba ikatuongezea milioni 150 kwenye vifaa tiba, Halmashauri ikaongeza milioni 70 kwa ajili ya jengo la mama na mtoto,miradi ni mingi najivunia tumetekeleza miradi 45 yenye thamani ya bilioni 2.6.Pia tumefanikiwa kupata umeme mtaa wa Iseni ambao awali haikuwepo pia Halmashauri imeendelea kutengeneza barabara ndani ya mitaa ya Kata yangu na tumetekeleza Ilani ya CCM kwa asilimia 100,”.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Kisiwa cha Bezi,James John,amesema zahanati hiyo ikikamilika itasaidia zaidi ya wananchi 6,000 wa Kisiwa hicho,waliokuwa wanakabiliwa na changamoto ya kupata huduma ya afya.

Mmoja wa wananchi wa Mtaa wa Kisiwa cha Bezi,Bezi Julius Ntenganija, amesema vifo vya wajawazito vilikuwa vingi ndio sababu ya kuomba zahanati ijengwe mtaani kwao.
“Matarajio yetu baada ya kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hii ni kupunguza vifo vya mama na mtoto na kutoa huduma ya afya kwa wananchi wote,kwani tulikuwa tunatumia takribani saa tatu kufuata huduma za afya ng’ambo na gharama ni kubwa,”.
Huku Maria Samweli,amesema, wajawazito walikuwa wanapotezwa maisha kwani ikitokea ameumwa uchungu usiku,muda wa kutafuta mtumbwi umsafirishe mpaka nchi kavu kisha uchukue usafiri mpaka kutoa cha afya cha Kata ya Sangabuye,ilikuwa inachukua muda mrefu.
“Lakini zahanati ikiwepo hapa usumbufu hatutauona kwani mtu akiugua ghafla unamuwaisha haraka anapata matibabu,”.
More Stories
MUWSA yatekeleza agizo la Rais Samia, yafunga mita za maji za ‘Prepaid’ 460
ETDCO wakamilisha mradi wa Kilovolti 132 Tabora – Urambo
Mgodi unaomilikiwa na Wakinamama wachangia Shilingi Milioni 800