January 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dimpoz azuru Macca kufanya Ibada ya Umrah

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva Omari Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz, amezuru mji wa Macca kufanya ibada ya Umrah kwa ajili ya kumuomba Mwenyezi Mungu amtakaze na mambo ya hovyo ya kidunia.

Akiweka picha yake kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka kuwa, amefanikiwa kusafiri hadi Macca na kufanya ibada takatifu ya Umrah jambo ambalo alikuwa ameliweka moyoni katika kutimiza ndoto zake.

“Alhamdulillah, Mwaka Juzi nilitamani kuwa mahali hapa kwa ajili ya ibada takatifu ya Umrah, lakini kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu haikuwezekana nikaishia kulazwa tena kitandani lakini sikufa moyo kwani Mwenyezi Mungu yeye ndiye mpangaji wa kila jambo na anapokupa mitihani basi jua ni kipimo cha imani yako kwake.

“Sina mengi zaidi ya kujiombea Dua na kuwaombea watu wote Allaah atujaalie kila jema tunalomuomba, atupe afya na uzima, atuondolee dhiki atupe na faraja, atuzidishie ridhiki, atusamehe madhambi yetu, apokee funga zetu, atuzidishie upendo miongoni mwetu. Inshaallaah,” ameandika Ommy Dimpoz.