Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Wasafi Media hapa nchini, Diamond Platnumz amewajibu wanaotaka aondolewe kwenye tuzo za BET, akisema ni mawazo yao na anayaheshimu.
Wanaompinga msanii huyo kupitia mitandao ya kijamii wanadaiwa kufanya hivyo ili kuonesha hisia zao kutokana na msanii huyo ‘kushiriki siasa akikiunga mkono chama tawala cha CCM’ nchini, kilichoshinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 unaolalamikiwa kuwa ulikuwa na udanganyifu.
Hata hivyo tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania imepinga madai haya na kusema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
“Epuka sana kumchukia mtu anayezungumza kitu kibaya juu yako, huwezi kujua, kaamka leo kavurugwa hasira zake kakumalizia wewe, kesho mwenyewe akikaa atajuta na kukuomba msamaha. Mimi naheshimu mawazo ya kila mtu, mtu akinifurahia, akinitukana akinisema mimi nashukuru”, amesema Diamond kupitia kituo cha Wasafi TV.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio