December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diamondplatnumz kufanya Kolabo na Diljitdosanjh

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Wasafi Media

Diamondplatnumz, ametangaza kufanya Kolabo na msanii

kutoka nchini India Diljitdosanjh.

Akithibitisha Kolabo hiyo kupitia kwenye Ukurasa wake

wa Instagram, baada ya Kupost baadhi ya picha akiwa

Studio na Msanii huyo.

Diamond amesema, tuamini muda si mrefu atatoa ngoma

mpya aliyomshirikisha Diljitdosanjh na kuwataka

mashabiki wake kukaa mkao wa kula.