December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diamond atakiwa kutoa wimbo mpya

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

KAKA wa msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamondplatunumz, Romyjons amemuomba msanii huyo kutoa wimbo mpya baada ya kukaa kimya takribani miezi sita.

Akitoa ombi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Romyjons amesema, mara ya mwisho Diamond kutoa wimbo ni ‘Waah’ aliyomshirikisha mkongwe wa muziki wa dansi kutoka nchini Congo Koffi Olomide.

“Diamond, Mimi kama Kaka yako na Watanzania kwa Ujumla tunaomba utoe nyimbo,” amesema Romyjons kupitia kwenye Ukurasa wake a Instagram.