Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Wasafi Media, Diamondplatnumz amemshukuru aliyekuwa mtangazaji wa kpindi cha michezo Wasafi FM, Maulidi Kitenge ambaye leo ameamia rasmi katika redio yake ya zamani EFM.
Akitoa shukrani hizo mara baada ya kuagana Diamondplatnumz amesema, amemshukuru Kitenge kwa kuiwezesha Wasafi fm kuwa redio nambaro moja hapa nchini kwa mujibu wa ripoti.
“kwanza kabisa nikushukuru kwa mchango wako mkubwa Katika taasisi ya Wasafi Media, kwa kuwa nasi bega kwa bega kuanzia Media changa mpaka leo imekuwa Media Nambari Moja Nchini katika kila report. Hakika haikuwa rahisi, shukran sana na sasa nina Amani ukirudi nyumbani.
“Mbali ya ushiriki wako kwenye Media, siku zote umekuwa ni kama kaka ama mjomba kwangu na ninakuahidi kwenda kwa kasi ileile ambayo siku zote umenisihi kuifanya, ili kutimiza Malengo ya Wasafi Media kuwa chombo kikubwa cha Habari Africa na kulipa Heshima Taifa letu. Mauldi Kitenge Kocha Mchezaji kwaheri,” ameandika Diamondplatnumz.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio