Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
MKURUGENZI mpya wa Halmashauri ya Wilaya Mbeya Erica Yegella,amesema serikali lazima iishi kwa vitendo na dhana ya kazi iendelee kwa kuhakikisha watumishi wanatoka ofisini na kwenda kuwatumikia wananchi ikiwemo kumalizia miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea na kuendelea na utekelezaji miradi iliyopo.
Aidha Yegella amesema kuwa kila mtumishi anawajibu wa kuwatumikia wananchi badala ya kusubiri kusukumwa kufanya kazi.
Yegella amesema hayo Januari 29,2025 wakati Akizungumza kwenye mkutano wa baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ulioshirikisha watumishi,Madiwani na viongozi wengine wa serikali.
Aidha Yegella amesema kuwa baada ya kuripoti katika Halmashauri ya Mbeya, tayari amefanya kikao na watumishi hasa idara ya mipango na kuwasisitiza kwenda kufanya kazi kwa weledi na uadilifu kwa maslahi mapana ya wananchi ambao ndio walipa kodi.
“Ndugu zangu watumishi tufanye kazi kwa ushirikiano mkubwa na uadilifu ikiwa ni pamoja na kuangalia changamoto za wananchi na kusimamia miradi ya maendeleo inahitaji kutekeleza”amesema Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mbeya, Mwalingo Kisemba, amewashukuru waheshimiwa madiwani wa Halmashauri yake kwa kushirikiana na wataalam kwenye maeneo yao kuendelea kufanya kazi na usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwalingo amesema kwamba ipo miradi ya maendeleo ambayo inatakiwa kutekelezwa hivyo ni vema Madiwani kwa umoja wao wakawa na ushirikiano ili kuweza kufanya kazi pamoja .
More Stories
TARURA Kilindi kutumia bil.5.2 bajeti 2025/26
Madiwani Kilindi wapitisha bil.36.8 bajeti 2025/26
THBUB yatoa tamko kulaani mauaji ya Jumanne Juma