Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online, Mbeya
KAMISHNA wa kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya Dkt Peter P Mfusi Amesema kuwa taasisi hiyo ipo chini ya ofisi ya waziri mkuu ambapo iliazishwa mwaka 2017 na lengo lake kubwa ni kuimarisha vita dhidi ya dawa za kulevya.
Amesema Mamlaka inafanya kazi yake kwa kufuata mikakati minne ambapo mkakati wa kwanza ni kuhakikisha kwamba inapunguza uingiaji ,uzalishaji na usambazaji wa dawa za kulevya nchini,pia kutoa elimu kwa jamii ili jamii iwe na uelewa mpana juu ya madhara yanatokana na dawa za kulevya kwani wakisha kuwa na uelewa mpana juu ya madhara yanayotokana na dawa hizo hawatajiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Kamishna Mfusi ameyasema hayo leo Agosti 5 jijini Mbeya kwenye maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani humo Ambapo amesema mkakati mwingine ni kupunguza madhara yanayotokana na madawa za kulevya nchini na katika mkakati huo kwanza wanatoa elimu kwa jamii wa dawa hizo kuhakikisha kwamba hawatumii dawa hizo ili wasipate madhara makubwa na kitu kikubwa kinachofanywa na mamlaka ni kutoa matibabu.
Ameongeza kuwa Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya inasimamia utoaji wa tiba kwa wathirika wa dawa za kulevya na kwakufanya hivyo kwa mfano kwa sasa wanavituo kama 15 ambavyo vimesambaa maeneo mbalimbali ya nchi ambavyo vyote kwa pamoja viliweza kusajili walaibu 12000 waliothirika na dawa za kulevya kwahiyo wanatoa matibabu kwa wa athirika wa dawa hizo za kulevya.
Kamishna Amefafanua kuwa mkakati wa nne nikuimarisha ushirikiano kikanda na na taifa kwasababu dawa za kulevya ni biashara inayovuka mipaka na wauzaji wadawa za kulevya hawana mikapa unakuta wanaishi Dar es Salaam lakini wanafanyabishara huko china hivyo wanawasiliana na wezao katika hizo nchi ilikuwaambia na kuhakikisha kwamba wanawadhibiti hao wauzaji wa dawa za kulevya.
” Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ipo hapa katika viwanja vya nanenane ili kuweza kutoa elimu kwa jamii juu ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba mkakati wetu wa pili ni kupunguza uhitaji wa dawa za kulevya nchini kwahiyo sisi kazi yetu nikutoa elimu hivyo tunawakaribisha wananchi wote wa mkoa wa mbeya waje katika banda la Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa ili kupata elimu.”amesema Kamishna Mfusi
“Wajitokeze ili kuweza kupata elimu sahihi juu ya biashara na madhara na matumizi ya dawa za kulevya ili waweze kuwashauri watu wanaowazunguka wasijiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya tunaelewa kwamba wanaokuja hapa wengi wao ni wakulima wanakuja kujifunza mbinu mbalimbali lakini tunaasa wakulima kwamba wasijishughulishe na mazao haya ambayo hayatakiwa ,wasijushughulishe na kilimo cha mirungi kwani ni mazao halamu na yanadhibitiwa kisheria na bora mtu aweze kulima mazao mengine ya chakula na biashara ambayo una uhakika wa kuvuna.
Kamishna Mfusi Ameongeza kuwa kama wakulima hao watalima bangi au mirungi basi wajuwe uhakika wa kuvuna ni mdogo na pia unaweza ukavuna na kuweka nyumbani kwako lakini Mamlaka ikakufikia ukakamatwa na ardhi uliyotumia kulima hayo mazao itataifishwa na Serikali lakini pia kuna vifungu virefu vya miaka 30 hadi vifungu vya maisha vitakuhusu.
“Kwahiyo wananchi wote wajitokeze ili kujionea kazi zinazofanywa na Mamlaka yao lakini pia aina mbalimbali za dawa za kulevya zilizoletwa kwenye maonyesho haya kwa maana kwamba wakiziona mahala popote wajue hizo ni dawa za kulevya.”amesema Kamishna Mfusi
Amesema kuwa wananchi wasikubali kudanganywa wakadhani ni pipi au kama kuna mtu wanajua anauza waripoti kwenye mamlaka na kwa kupiga namba bure kabisa ambayo ni 119 piga namba hiyo na utambulisho wako hautaonekana na utakuwa huru bila wasiwasi kabisa hivyo wanachi wote wajitokeze kwenye maonyesho hayo ya nanenane na wakulima wajihusishe na kilimo cha mazao halali na si vinginevyo.
More Stories
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu