May 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DCEA yajivunia uadilifu vita dawa za kulevya

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

imejivunia weledi mkubwa walionao watumishi wa mamlaka hiyo, hivyo hawawezi kushiriki vitendo vya rushwa pindi wanapotekeleza majukumu yao.

Akijibu maswali ya wahariri wa vyombo vya habari wakati wa semina iliyoandaliwa na mamlaka hiyo kwa wahariri hao Jijini Dar es Salaam jana Kamishina wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya( DCEA) Dkt. Peter Mfisi, amesema;

“Watendaji wa Mamlaka yetu wanawezeshwa vizuri kutimiza majukumu yao, ndiyo maana wapo makini na hawashiriki vitendo vya rushwa.

Kwa kweli katika kitengo chetu cha Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, wafanyakazi wanawezeshwa vizuri, hivyo hawawezi kujihusisha na vitendo vya rushwa.”

Kamishina wa Hudumaza Taasisi- DCEA (wa pili kutoka kushoto), akiwa na Wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini, wakifuatilia mada wakati wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) leo Novemba 13, 2023.

Amekiri kuwa, wauzaji wa dawa za kulevya wana mbinu nyingi, lakini pia wana hela sana hivyo wanaweza kukushawishi kwa vyovyote hata kutaka kukupa sh. milioni 60 ili waachiwe waendelee na biashara zao, lakini mwisho wa siku vijana wetu ndiyo wanaoangamia na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

“Mimi nimebakiza miaka miwli ya kustaafu, halafu anatokea mtu anakupa sh, Mil. 60 ili umuachie, ukiangalia maokoto ninayolipwa na kile ambacho nitalipwa baada ya miaka miwili nikistaafu ni nyingi kuliko milioni 60, kwa hiyo siwezi hata siku moja nikafanya hivyo,” alisema Dkt. Mfisi na ameongeza;

“Lakini pia kwenye mamlaka yetu wapo watu kutoka vitengo mbalimbali, kwa hiyo mnapokwenda kumkamata mtu mnakuwa hamjuani, haujui huyu katoka kitengo gani, mwisho wa siku wote mnakuwa mnaogopana, vinginevyo mwisho wa siku utakamatwa tu na kupoteza kibarua.”

Dkt. Mfisi amesema, kutokana na mazingira hayo vitendo vya rushwa havipo, kwani hata hata anayehamishiwa kwenye mamlaka hiyo, mazingira ya kazi anayokutana nayo yanakuwa ni tofauti na alikotoka, hivyo ni lazima atafanyakazi kwa weledi.

Wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini wakisikiliza mada mbalimbali wakati wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) leo Novemba 13, 2023.