December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Tukai akabidhiwa zawadi ya Mbuzi Wilayani Nzega

Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Nzega

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Luteni Mstaafu Maganga Sengerema pamoja na viongozi mbalimbali wa Jumuiya za CCM, wamemkabidhi zawadi ya mbuzi Mkuu Mpya wa Wilaya hiyo Naitapwaki Lemeya Tukai kama sehemu ya mapokezi rasmi, alipokwenda kusaini vitabu katika Ofisi za CCM Nzega.

Mh.Sengerema alisema wamefurahi kupata Mkuu wa Wilaya hiyo Naitapwaki Lemeya Tukai ambaye pia ni mama kama aliyetoka Wilaya hiyo kuelekea Biharamulo Mh.ACP Advera Bulimba.

” Tunamshukuru Mh. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Kwa kutuletea wewe kuwa Mkuu wa Wilaya hii ya Nzega, lakini pia tukupongeze Kwa kuteuliwa kwako mh.Mkuu wa Wilaya, wewe ni mama na kama inavyofahamika siku zote kazi ya mama ni kulea familia, tunaamini atailea Nzega yetu, hakika tumefurahi sana kupata Mkuu wa Wilaya hiyo Naitapwaki Lemeya, maana aliyeondoka kuelekea Biharamulo ni mama Mh.ACP Advera Bulimba na aliyekua ni mama pia, basi ni jambo la kumshukuru sn Mwenyezi Mungu” alisema Mh.Sengerema.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya Mh.Naitapwaki Lemeya Tukai alisema amefurahi kukutana na viongozi wenye mapenzi mema hususani Kwa zawadi ya mbuzi ambayo ameipata.

“Mh. Mwenyekiti bosi wangu, Mimi kama nilivyokwambia Toka nilivyoipitia hapa Nzega kuwa Mimi nimetokea kwenye Chama, na nilitokea UWT nikaja kwenye Chama na sasa namshukuru sn Mh.Rais Kwa kuniona naweza kumsaidia majukumu yake katika Wilaya hii ya Nzega, najua ameniamini nami nitaendelea kuzilinda heshima hii ambayo sitakubali mtu mwingine yeyote aje aivunje, hivyo niwatoe hofu kuwa CCM naijua” alisisitiza Mkuu huyo.

Aidha alisema kikubwa apewe ushirikiano ili aweze kutekeleza vema majukumu aliyopewa katika kuhakikisha Wilaya ya Nzega inasimama kikamilifu kimaendeleo.

Hata hivyo aliongeza kuwa wakati Sasa umefika wa kila kiongozi au mwanachama wa CCM kuhakikisha anatekeleza wajibu wake ama majukumu yake kisawasawa ili kuweza kumrahisishia kazi mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Tukai alisema Kwa upande wake atahakikisha anatoa ushirikiano wake wa dhati katika kuhakikisha CCM inaendelea kuwa imara zaidi ya jana, kwani yeye ametokea katika Chama Cha Mapinduzi ( CCM )