November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC.Shekimweri:jitokezeni kushiriki Matembezi marathon kutangaza utalii wa ndani

Na Zena Mohamed, Timesmajira Online, Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabiri SHEKIMWERI,ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio za Mtembezi Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika July 7 mwaka huu zenye lengo la kutangaza utalii wa ndani wa Mkoa huo.

JABIRI ametoa rai hiyo wakati akizindua jezi ambayo itatumika katika mbio hizo nakusema kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na Mtembezi Adventure wamekubaliana kufanya mbio hizo zitakazo ambatana na kutangaza utalii wa ndani pamoja na kuutangaza Mkoa wa Dodoma.

“Mkoa wa Dodoma una utalii mwingi kuna utalii wa ngoma,utalii wa kilimo kwa maana ya zabibu na mapori ya akiba, mji wa serikali Mtumba, barabara ya mzunguko na vingine vingi vya kiutamaduni ambavyo vinavutia hivyo kufanyika kwa mbio hizo kutasaidia kutangaza utalii uliopo ndani ya mkoa wetu, niwaalike wananchi wa Mkoa huu kujitokeza Kwa wingi kushiriki mbio hizo,”.

Aidha Jabiri aliongeza kuwa siku tatu kabla ya mbio hizo kutakuwa na shughuli mbalimbali ambazo zitakuwa zikionesha utalii wa Dodoma.

“Tutakuwa na maonesho ya vitu mbalimbali vya kitalii kabla ya mbio hizo katika Capital City hivyo wananchi kujitokeza kuja kuangalia maonesho hayo,”.

Naye Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa TANAPA, Dkt, Noel Myonga amesema wanatambua thamani ya michezo katika kutangaza utalii nakuomba utalii huo uambatane na kutangaza utalii wa kawaida kwani inachangia kwa kiasi kikubwa kutangaza utalii.

“Tunatamani utalii huu uambatane na utalii wa kawaida kwa kuwa hapa pia tuna mambo mengi ya kitalii,kuna utalii wa kilimo,utamaduni na chakula hivyo tuko tayari kushirikiana na wadau mbalimbali kutangaza utalii wa ndani,”.

Mkurugenzi wa Mtembezi Adventure Samson Samweli,amesema wameandaa Mtembezi Marathoni mkoani Dodoma kwa ajili ya kuhamasisha utalii wa ndani wa Mkoa huo.

“Mtu anaweza kuuliza kwanini tumeandaa mbio hizi Dodoma kunautalii gani?, Dodoma kunautalii mwingi sana ,unaotokana na shughuli za kijamii kama kilimo na tamaduni, mapori ya akiba na nyingine nyingi”.

Kuhusu zawadi zitakazotolewa , kwa washindi watatu,Samson amesema zitatolewa na kampuni ya gesi ya Orxy mbio za kilomita 21,10 na kilomita 5.