Na Mary Margwe Naisinyai-Simanjiro
MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Dkt.Suleiman Serera, ametoa agizo Kwa wananchi Wilayani humo kuhakikisha kila kaya inapanda miti 10 ili kulinda Mazingira yanayoendelea kuharibika kila kukicha.
Hayo alibainisha jana wakati alipokua akizungumza kwenye uzinduzi wa upandaji miti, ambapo Kiwilaya ilifanyika katika Kijiji cha Naepo Kata ya Naisinyai mbele ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo Kiria Ormemei Laizer, mfanyabiashara maarufu wa Madini ya Tanzanite Mji Mdogo wa Mirerani Saniniu Laizer, Diwani wa Kata hiyo Taiko kurian Laizer.
Dkt.Serera amesema ili kuhakikisha Mazingira yanakua !azuri na ya kuvutia ni wakati sasa umefika wa kila mwananchi kuona umuhimu wa kupanda miti bila kushurutishwa ili kuboresha Hali halisi ya Mazingira.
Amesema kupanda miti ni jambo moja na kuitunza miti ni jambo lingine, hivyo kila kaya ijitahidi kuhakikisha imepanda miti 10 ikiwa ni sambamba na kuitunza na si vinginevyo.
” Mazingira yetu yameharibika sana kutokana na suala la mifugo na kilimo mifugo, hivyo kufuatia hili sasa ni lazima tubadilike juu ya hili, katika kaya zetu tukiweza angalau kupanda miti 10 na kuitunza naamini rasilimali misitu itarudi na Mazingira yataboreka na kuwa bora zaidi na ya kuvutia ” amesema Dkt.Serera.
Aidha Dkt.Serera amesema miti itaendelea kutafutwa kwa wingi bila gharama yoyote, ambapo aliwahakikishia wananchi kutokua na wasiwasi kwani miti ipo na itaendelea kuwafikia kaya hadi kaya kaya.a
” Kwahiyo sisi huku Wilayani tutakaa na watendaji wa Kata na Vijiji tujue idadi ya kaya zenu tunazopeleka hii miti 10, anzeni kuwahamasisha wananchi juu ya hilo huku wakisubiria kupatiwa hiyo miti na hatimaye tuweze kulikamilisha hili Kwa asilimia 100″ amesema Dkt.Serera.
Amesema misitu inatajwa kuwa ndio rasilimali muhimu kuliko zote duniani katika maisha ya binadamu chakushangaza ndio inayoongozwa kuathiriwa na kuharibika Kwa kasi kubwa na Watu, kwani miti inayopandwa ni michache ukilinganisha na inayovunwa.
” Hongereni sana wenzetu wa maliasili na Wakala wa hudumaza Misitu Tanzania (TFS) Kwa kuanzisha vitaku mbalimbali Kwa ajili ya kuhakikisha tunatoa miti katika Wilaya yetu,kwasababu eneo hili ni la Madini na tunayo maeneo mengi ya madini katika Wilaya yetu,tuweze kupanda miti ya kutosha, kwahiyo Afisa maliasili utamjulisha Afisa Madini Mkazi Mirerani juu ya huo utaratibu” amefafanua Dkt.Serera.
Mbali na kupanda miti 10 Kwa kila kaya, pia amezitaka Taasisi mbalimbali kuhakikisha katika maeneo ya Ofisiza watendaji wa vijiji na Kata, shule wanapanda miti ya vivuli pamoja na miti ya Matunda kwaajili ya kupata lishe, kwa kufanya hivyo miti itakua imebireshwa ambayo ndio uhai wenyewe inayotoa hewa nzuri, kuleta mvua.
” Nimesikia na nimemuagiza Meneja wa TFS , hatukatai kuanzisha shughuli zingine za Uchumi kuna watu wanaenda kufungua nankatikanufunguaji wa mashamba Mwenyekiti wa Kamati ya uvunaji katika ngazi ya Wilaya ni ni Mkuu wa Wilaya na mimi nimeweka utaratibu kabla sijaruhusu barua ya kufungua shamba, barua hiyo ni lazima ipite Kwa Mtendaji Kijiji, yeye ndio atathibitisha pale kwamba eneo hilo ni kweli ni la mtu husika anataka kufungua shamba ,lakini la pili barua hiyo pia itapitia kwa Meneja wa TFS” amesisitiza Mkuu wa Wilaya hiyo.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja