Na Steven Augustino, Times Majira Online, Tunduru
MKUU wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amepiga marufuku vitendo vya Polisi kufanya oparesheni za usiku kwa kukamata madereva pikipiki zinazo fanya biashara ya ubeba abiria kwa kisingizio cha ukaguzi wa leseni na askari wa usalama barabarani kukamata vyombo vya moto wakiwa wanatokea mafichoni unaendela hivi sasa.
Mtatiro alitoa tamko hilo wakati akiongea na wadau wa usafirishaji wa pikipiki na bajaji katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Balaza la Idd mjini hapa.
Amesema kuwa hali hiyo imefutia tukio la operesheni iliyofanyika usiku wa kuamkia Desemba 14, mwaka huu, ambapo baada ya kupokea malalamiko ya unyanyasaji huo alienda Polisi saa 7.15 usiku na kuwatoa madereva pikipiki 24.
Mtatiro ambaye ameonekana kuwa na hasira kutokana na kukerwa na tukio hilo alimtaka Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tunduru (OCD) na timu yake kukaa, kujipanga na kutengeneza utaratibu wa kutoa elimu kwa madereva hao na kuwatafutia leseni kwa ghalama isiyo zidi shi.70,000 katika kipindi cha miezi mitatu cha kuanzia Januari hadi Machi mwakani ili kuondokana na kero za kusumbuana na madereva wasio kuwa na leseni.
“Mimi kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya nataka kuona operesheni za Polisi zinakuwa na weledi zinazoendana na utoaji wa elimu ya usalama barabarani ili kupunguza ajali,”amesema.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea