November 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Mpogolo “Nitatumia siku Saba kushughulikia kero 26 za wananchi Ukonga

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar

MKUU wa Wlaya ya ilala, Edward Mpogolo, amemuhakikishia Katibu wa NEC, Siasa, itikadi, Uenezi na mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla, kutumia muda wa siku saba kuzishughulikia kero 26 zilizowasilishwa na wananchi wa Chanika katika Jimbo la Ukonga.

Mpogolo, ameyasema hayo mara baada ya kukabidhiwa kero hizo na CPA Makalla, ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Chanika, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara ya Mwenezi huyo, ambapo leo alikuwa katika Jimbo la Ukonga.

Amesema, kero zote 26 alizokabidhiwa, atatumia muda wa siku saba (wiki Moja) kuzipatia ufumbuzi, ambazo kati ya kero hizo zimegusa upande wa afya, miundombinu, ardhi, ajira, mazingira na huduma nyingine za kijamii.

Awali akizungumzia utekelezaji wa ilani katika Wilaya ya Ilala, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kujipatia Wilaya hiyo fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika sekta zote.

Pia, akizungumzia kuhusu ongezekezo la ukusanyaji wa mapato katika Wilaya hiyo, ameeleza kuwa, Wilaya ya Ilala imekuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato kwa kiwango cha juu ambapo hivi sasa imeweza kukusanya zaidi ya Bilioni 111 fitauti na iliyokuwa awali, huku akieleza kuwa fedha hizo zimekuwa zikitumika katika kuwapelekea wananchi miradi ya maendeleo huku akieleza Wilaya hiyo imepokea kiasi cha Shilingi Bilioni 200 kutoka kwa Rais kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.