October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC.Mpogolo kutumia siku saba, kushughulikia kero 26 za wananchi Ukonga

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar

MKUU wa Wlaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amemuhakikishia Katibu wa NEC, Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa, CPA Amos Makall kuwa atatumia siku saba kushughulikia kero 26 zilizowasilishwa na wananchi wa Chanika Jimbo la Ukonga.

Mpogolo, ameyasema hayo mara baada ya kukabidhiwa kero hizo na CPA Makalla, ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar- es-Salaam, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa shule ya sekondari Chanika, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara ya Mwenezi huyo, ambapo Julai 7,2024 alikuwa katika Jimbo la Ukonga.

Amesema miongoni mwa kero hizo ni pamoja na sekta ya afya, miundombinu, ardhi, ajira, mazingira na huduma nyingine za kijamii.

Awali akizungumzia utekelezaji wa ilani katika Wilaya ya Ilala,amesema Wilaya hiyo imepata fedha nyingi za miradi ya maendeleo kwa sekta zote.

Pia ameeleza kuwa Wilaya hiyo imekuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato kwa kiwango cha juu ambapo hivi sasa imeweza kukusanya zaidi ya bilioni 111 tofauti na iliyokuwa awali.

Huku akieleza kuwa fedha hizo zimekuwa zikitumika kwa ajili ya kupeleka miradi ya maendeleo kwa wananchi huku Wilaya hiyo imepokea kiasi cha bilioni 200 kutoka serikalini kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.