December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Mpogolo awatunuku vyeti madereva zaidi ya 1000

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online. Dar

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amewatunuku vyeti vya uthibitisho madereva zaidi ya 1000 waliofanya mtihani na kuthibitishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).

Hafla ya ugawaji vyeti hivyo umefanyika Juni 4, mwaka huu, katika Ukumbi wa mikutano Arnaoutoglou jijini Dar es Salaam, ambapo Mkuu huyo wa Wilaya alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.

Hata hivyo, hafla hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo madereva, kamati ya Uthibitishaji wa madereva, Usajili wa wahudumu, Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na vyama vya wasafirishaji.

Mpogolo amewataka madereva hao kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa manufaa yao na abiria, huku akiwasisitiza madereva ambao hawajathibitishwa kujitokeza ili wathibitishwe.