DC MPOGOLO AONGOZA KAMPENI YA USAFI ILALA
Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ameongoza Kampeni ya Usafi Wilaya ya Ilala kwa kusafisha eneo la Uwanja Ndege na Barabara ya Nyerere.
Akizundua Kampeni hiyo ya Usafi Ilala Leo Pamoja Wakandarasi wa Usafi waliojitokeza kuunga mkono Juhudi za Serikali ,Kampuni za Kajenjele ,Kampuni ya SATEK na KIMWEDE , Mkuu wa Wilaya Mpogolo alitoa agizo viwanda vya Barabara ya Nyerere na Kampuni zilizopo Barabara hiyo kupaka Rangi majengo na kupendezesha maeneo yao.
Akitoa agizo hilo leo alisema kampeni ya usafi Wilaya ya Ilala inaunga mkono agizo la Mkuu wa Mkoa la kupendezesha mji wa Dar es Salaam kuweka maeneo yote katika hali ya Usafi.
“Naagiza makampuni ya Barabara ya Nyerere na viwanda wakikishe yanapaka Rangi majengo yao kwa ajili ya kupendezesha Mji wetu Kila wakati uwe msafi ” alisema Mpogolo .
Wakati huo huo alitoa agizo kwa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam kuboresha K
Kwa kutunza Mazingira barabaraba ya Nyerere mpaka Ikulu Wilayani Ilala .
Katika hatua nyingine alisema kesho kutwa tunatarajia kupokea ugeni mzito katika nchi yetu Makamu wa Rais wa Marekani anafanya ziara ya kikazi hapa nchi hivyo tuakukikishe tunatunza mazingira kwa usafi ,ugeni Makamu wa Rais wa Marekani ni fursa kwa nchi yetu Tanzania .
Meneja Mahusiano Benki ya Kanda ya Dar Es Salaam Irene Masaki, alisema usafi iwe tabia yetu maelekezo yaliotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala wameyapokea watatekelezwa.
Diwani wa Viti Maalum Magreth Cheka alisema suala la usafi iwe endelevu Wilaya ya Ilala Wananchi tufanye Kila wakati .
Diwani wa Kipawa Idani Kwezi alisema Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ni mchapakazi Wana Ilala tushirikiane naye katika kudumisha usafi pamoja na kuleta maendeleo .
Diwani Aidani Kwezi alisema kampeni ya usafi iwe Kila siku ikifika mwisho wa mwezi kampeni inaitimishwa .
“Kata yetu ya Kipawa tupo katika Kampeni endelevu ya Kipawa ya Kijani tumejipanga kupanda miti 10000 Kwa ajili ya kusaidia serikali kutunza Mazingira Yetu ” alisema Idani .
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa