Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
MKUU wa Wilaya ya Mbeya,Beno Malisa ameagiza Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Watendaji wa Kata na Vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kuwasilisha ripoti ya mahudhurio ya wanafunzi wa kidato cha kwanza na darasa pamoja na awali kwa mwaka wa masomo 2025, ili kubaini wasioripoti shule.
Akizungumza Februari 11, 2025 wakati alipotembelea shule ya Sekondari Ihombe na Juhudi Usongwe Malisa amesema ili kuangalia maendeleo ya mahudhurio ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza ambapo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya mahudhurio yamefikia asilimia 81% hadi mwezi Februari, Wanafunzi walioripoti kwa shule zote 40 za sekondari zilizopo katika halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Malisa amewaagiza Watendaji wa kata na vijiji kushirikiana na Wazee wa kimila na Viongozi wa dini ili kufanikisha zoezi hilo na hatimaye kufikia asilimia 100% ya wanafunzi wote wanaotakiwa kuripoti shule.
“Kama alivyoagiza Mkuu wa Mkoa kuwa watoto wanaoingia kidato cha kwanza wazazi wawapeleke shule na kusiwe na kisingizio cha nguo za shule, kama hana nguo za sekondari avae shule za shule ya msingi alikotoka, tunachohitaji ni watoto kuanza masomo mapema” amesema Malisa.
Malisa amesisitiza kuwa kwa wazazi ambao hadi sasa watoto wao hawajafika shuleni watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Ameviagiza vyombo vya kisheria kushghulika na wazazi ambao hawajawapeleka watoto shule.
Mkuu wa Polisi wilaya ya kipolisi Mbalizi SSP Mathew Mgema, amesema Polisi wilayani Mbalizi itahakikidha inashirikiana na watendaji wa kata na askari kata kuwachukulia hatua wazazi na walezi watakaoshindwa kuwapeleka shule watoto wao kuanza masomo hasa ya sekondari.
SSP Mgema ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuhakikisha wanawapeleka watoto shuleni kabla ya kufikiwa na mkono wa dola kwani elimu ni kwa faida yao na Taifa kwa ujumla.
Maafisa elimu kata za Iwindi, Utengule Usongwe na Nsalala wameahidi kuhakikisha wanaendelea kuhimiza watoto kutambua umuhimu wa elimu na wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shuleni kuanza masomo ya sekondari na kuchukua hatua kwa watakaoshindwa kuwapeleka shule watoto wao.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/img-20250212-wa02288039571504369430541-1024x472.jpg)
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/img-20250212-wa02298770349165877969245-1024x682.jpg)
More Stories
Dkt.Mpango aagiza mfumo wa NeST utumike kudhibiti ubadhirifu,aipongeza PPRA
Mpogolo ashauri Ilala kutenga bajeti ya mazingira
Sheria mpya nguzo ya uwekezaji kuongezeka nchini