Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza Amina Makilagi ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), kuhakikisha inafanya kazi ndani ya muda uliopangwa ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma kwa wananchi katika mradi wa ujenzi wachanzo kipya cha maji Butimba.
Mradi huo ambao mpaka sasa umefikia asilimia 94 ya utekelezaji wake hali ambayo imemfurahisha Mkuu huyo wa wa Wilaya ambaye ametumia fursa hiyo kuipongeza Mwauwasa kwa kadi hiyo ambayo inawapa Matumaini kuwa ndani ya muda na huduma ya maji itapatikana kama ilivyo lengo.
Hayo ameyasasema Agosti 26, 2023 wakati wa ziara ya kukagua mradi huo eneo la Butimba ambapo ameeleza kufurahishwa na maendeleo ya mradi huku akieleza kwamba hatua iliyopigwa ni kubwa huku akiwasisitiza MWAUWASA kufanya kazi kwa muda ili kupunguza changamoto ya hupatikanaji wa maji kwa wananchi
“Tunawashukuru na kuwapongeza MWAUWASA kwa utendaji wenu wa kazi nzuri kwa kipindi kifupi tumeona mabadiliko makubwa katika utekelezaji ,kwa kasi hii tunapata matumaini kwamba utekelezaji utakamilika ndani ya muda na huduma itapatikana kama ilivyokusudiwa,” amesema Amina.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA,Neli Msuya amesema amepokea maelekezo hayo na kuahidi kuendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo huku akieleza kuwa mpaka sasa umefikia asilimia 94 na kwamba kazi za ujenzi ziko katika hatua za mwisho.
“Hadi sasa kasi ya utekelezaji ni ya kuridhisha, tunafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha tunakamilisha kila hatua na tutafanya majaribio Septemba 15,2023 kama ilivyopangwa,” amesema Neli.
Mradi wa chanzo kipya cha maji Butimba unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benki ya Uwekezaji ya Ulaya na Shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa gharama ya bilioni 69.
Kukamilika kwa mradi kutaboresha na kuwezesha upatikanaji huduma ya majisafi kwa wakazi wapatao 450,000 waishio maeneo ya pembezoni.
More Stories
RC Mtambi awataka Maofisa kilimo kutoa elimu ya kilimo mseto
Rais Samia kuelekea nchini Brazil kushiriki mkutano wa G20
Rais Samia atoa maagizo ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo