Na Heri Shaaban
Mkuu wa Wilaya Ilala Arch,Ng’wilabuzu Ludigija amewagiza wasimamizi wa Barabara za Mijini na Vijijini Tarura kuwasimamia Wakandarasi wa Barabara za Mtaa wa Kichangani Kinyerezi kutokea Ulongoni ndani ya siku tano iwe imeshamalizika ifunguliwe.
Mkuu wa Wilaya Arch, Ludigija aliyasema hayo Dar es Salaam l
jana,katika ziara yake ya kikazi kuangalia athari za amvua zilizokata mawasiliano ya Barabara na madaraja
eneo la Zimbili kwa Masista na Kichangani Kinyerezi.
“Ninaagiza ndani ya siku tano Barabara ya Kinyerezi Kichangani kuelekea Ulongoni Ukonga imalizike Mawasiliano yaweze kurudi huduma za jamii ziendelee ” alisema Ludigija.
Ludigija alisema kalavati la awali lilikuwa dogo amewashauri TARURA waweke kalavati kubwa lipitishe maji kwa urahisi.
Wakati huo huo Ludigija amewapa wiki mbili watalaam wa TARURA kufanya Usanifu wa daraja kubwa litakalojengwa eneo la Kinyerezi Zimbili kwenda kwa Masisita ambalo linaunganisha mawasiliano Pugu Stesheni,Ulongoni na Kinyerezi.
Alisema Mara baada usanifu kumalizika ujenzi wake utaanza Mara moja linajengwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Hassan Suluhu.
Alisema Rais wetu Samia Haasani Suluhu ni Rais wa Wanyonge anatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kutatua kero za wananchi wake.
Diwani wa Kinyerezi Leah Mgitu amepongeza Serikali kuchukua hatua wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya llala Ludigija amefika na wataalam wa Tarura kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Barabara na madaraja.
Diwani Leah amewataka wananchi wake kuwa wavumilivu Serikali imeanza kujenga hivyo kwa sasa watumie njia mbadala kwa ajili ya kupitisha magari yao.
Mhandisi wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Joseph Mkinga alisema mafundi wanajenga usiku na mchana kuakikisha ndani ya siku tano alizotoa maagizo Mkuu wa Wilaya ya Ilala wawe wamemaliza kujenga na kuweka kalavati.
Mhandisi Mkinga alisema madaraja hayo yamekatika kutokana na nguvu ya maji kubwa na takataka ngumu ambazo zilikuwa zinasafiri na maji.
More Stories
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi
SACP Katabazi: Elimu ya usafirishaji wa kemikali bado ni muhimu kwa watanzania