May 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Karatu awaagiza madiwani kutoa elimu jumuiya za maji

Na Sophia Fundi, Timesmajira, Karatu

MKUU wa wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Dadi Kolimba amewataka madiwani kusimamia na kutoa elimu kwa jumuia za maji kufuata taratibu za serikali na kufanya kazi chini ya mamlaka za maji vijijini RUWASA.

Kolimba, ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na madiwani katika kikao Cha kawaida Cha Baraza la madiwani kilichofanyika Jana kwenye ukumbi wa hospitali ya wilaya.

Amesema, kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi wa vijiji wa serikali na wa Chama kutofuata taratibu za serikali za jumuia za maji.

Hata hivyo amesema, huko nyuma kulikuwa na jumuia za maji zilianzishwa katika maeneo yenu, serikali ikaja na sheria na taratibu za jumuia zote kuwa chini ya mamlaka za maji vijijini RUWASA lakini Kuna baadhi ya jumuia hazitaki kufuata taratibu za serikali.

Mkuu huyo wa wilaya amesema, jumuia hizo zimekuwa zikivunja taratibui za serikali ikiwemo baadhi kukusanya fedha za maji na kukaa nazo majumbani bila kupeleka benki, Jambo ambalo ni ukiukwaji wa Taratibu za serikali za mamlaka za maji vijijini RUWASA.

Amewataka, madiwani katika maeneo yao kusimamia suala hilo na kutoa elimu kwa jumuia hizo kufanya kazi chini ya mamlaka za maji vijijini RUWASA na fedha zote za maji zilipwe kwa kutumia Contro namba.

“Waheshimiwa madiwani Kuna baadhi ya jumuia hazifanyi kazi kwa kufuata taratibu za serikali, jumuia za maji zinatakiwa ziwe chini ya mamlaka ya maji vijijini RUWASA, hivyo katika maeneo yenu simamieni hilo,” amesema Kolimba.