December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC.Kalambo aishukuru benki ya NMB kwa msaada wa Mabati

Na Mwandishi Wetu,Kalambo.

MKUU wa Wilaya ya Kalambo,Tano Mwera ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada wa mabati 600 yaliyotolewa kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya Zahanati Wilayani hapa.

Mwera ametoa shukrani hizo wakati alipotembelea ukarabati wa Zahanati ya Kijiji cha Kapozwa ambapo shughuli za ujenzi zinaendelea.

Ambapo amebainisha kuwa, alifika Kijijini hapo siku za nyuma katika ziara zake za kawaida za kutembelea Vijiji hivyo ndipo alipata kero hiyo ya Zahanati kuezuliwa paa na kwa upepo mkali.

“Nilifika hapa na kuchukua kero hii, na kuomba msaada kwa Benki ya NMB, NMB Wakapokea kilio hicho na kutoa msaada wa Mabati 600.

“Pamoja na Zahanati hiyo kukarabatiwa, bati hizo pia zitatumika kukarabati Zahanati za Vijiji vya Mambwekenye na Mpanga…Kazi Iendelee” Amesema Mwera.

Aidha, Mwera amebainisha kuwa, Serikali inatambua changamoto mbali mbali hivyo wataendelea kuzitatua kwa nguvu zote ikiwemo kushirikiana na wadau wa sekta binafsi ikiwemo Benki hiyo ya NMB na wadau wengine katika kusaidia utendaji bora wa Rais wa Tanzania Suluhu Suluhu Hassan.