November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jokate: Tuenzi mazuri yanayofanywa na Samia

Na David John,Timesmajira online,Korogwe

MKUU wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Jokate Mwegelo amesema kuwa kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika kuboresha miundombinu za huduma mbalimbali ya afya lengo lake ni kusogeza huduma karibu zaidi na mwananchi.

Jokate ametoa kauli hiyo mei 28 mwaka huu baada ya kufanyika kwa mbio ambazo zilikuwa zimeaandaliwa kwa wanawake wajawazito wilayani humo na kupewa jina la Mamathon.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaguswa na changamoto mbalimbali hususani huduma za akina mama na mtoto na sisi kama viongozi vijana kupitia Mamathon tunaenzi yale mema na mazuri ambayo Rais wetu amekuwa akiyafanya kupitia Serikali yake ya Awamu ya sita kwa watanzania na zaidi kwenye kundi la akina mama na mtoto,

“Sisi ndio walezi wa jamii zetu, ndio wajenzi wa Taifa kwa maana ukizungumzia watoto wanatoka tumboni mwetu ndio maana kwa namna moja ama nyingine, akina mama ndio wanatunza hawa watoto japo akina baba nawenyewe wanasaidia kulea,”amesema.

Jokate amesema Korogwe waliandaa Mamathon ni mahususi kwa ajili ya kumsemea Rais Samia ambaye ameweika mbele ajenda za mwana mama na mtoto”Kwa hiyo hili tukio sio tukio tu la kutembea lakini kubwa muende kuwa mabalozi wa Rais Dkt Samia Hassan Suluhu kwani mwendo ameuaza vizuri ,mwendo atauendeleza na sisi wote tunatakiwa kuungana naye.”Amesema

Aidha amewaeleza akina mama wajawazito kuwa Serikali ya Awamu ya Sita lengo lake nikupeleka huduma za afya kwenye maeneo yao na kwa Wilaya ya Korogwe hakuna kata ambayo haina huduma hizo na kazi hiyo yote inafanywa na Rais Dkt Samia

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah na Meya wa Temeke mkoani Dar es Salaam Abdallah Mtimika wametumia nafasi hiyo kumpongeza Jokate kwa kufanya tukio la kuleta hamasa kwa wamama wajawazito kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah amesema jambo ambalo amelifanya Mkuu wa Wilaya Jokate ni kubwa na ni jambo la mama.

“Nimekuja hapa kwa niaba ya wakuu wa Wilaya wote Mkoa wa Tanga, tunampongeza kwani anaupiga mwingitangu ameingia wilayani Korogwe,”amesema.

Amesema wananchi wa Wilaya ya Korogwe wamelamba dume na kama ni madini basi ya Tanzanite ambayo yanazalishwa Tanzania peke yake.

Amefafanua kuwa Jokate ameupiga mwingi akiwa katika Wilaya ya Kisarawe,Temeke na Meya wa Temeke ametoa ushuhuda lakini kubwa zaidi amewaeleza wananchi wa Korogwe kwamba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewapendelea kwani amewapelekea jembe na sasa wanashuhudia Mamathon.

Amesema kupitia Mamathon , Jokate amefanya jambo kubwa kubwa linalogusa maisha ya wanawake wengi na wao kama viongozi wa mkoa wa Tanga wataendelea kumuunga mkono mkuu wa Wilaya hiyo ya Korogwe .

Nakuongeza kwamba “Tunauwezo wa kufanya mambo mengi Kwa muda mmoja na Mimi mwenyewe ni shuhuda kwani Kwa miaka minne nimezaa watoto wanne eeee akina mama hoyee kwahiyo mimi ni mjamzito Mstaafu na nimejifungua mwezi wa kwanza mwaka huu lakini haijazuia mimi kufanya kazi kama mkuu wa Wilaya ,kusoma ,kusimamia familia ,Wala masuala ya kiuchumi hivyo tunaupiga mwingi sana kwahiyo kama tunaweza kufanya yote haya tukiwa wajawazito tutashindwa kukimbia hivyo Leo akina mama wa Korogwe wameupiga mwingi sana “amesisitiza Mkuu wa Wilaya ya pangani Zainab

Pia amemuhaidi Mkuu wa Wilaya Jokate kwamba jambo hilo kubwa aliloliazisha litakuwa endelevu kwani atamuunga mkono popote alipo naye atakuwepo na Tanga wataendelea kumuunga mkono .

Hata hivyo kupitia hadhara hiyo alitoa salamu za Waziri wa Maji ambaye ni Mbunge wa Jimbo la pangani mkoani Tanga Jumaa Awesu kwamba Amesema kuwa kwakuwa anawapenda sana wanawake wa Korogwe changamoto ya Maji linakwenda kwisha lakini Yeye mwenyewe kama pacha wa Jokate ameweza kuchangia shilingi milioni tatu.

Pia amemuelezea Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda kwamba tangu ameshika nafasi hiyo ya uongozi amekuwa akifanya vizuri na wao kama wanawake watanzania wanamuunga mkono na wanamemuhakikishia kwamba popote alipo Mwenyekiti huyo wa wanawake taifa na wao kama vijana wake ajuwe wapo pamoja naye .