Na Hadija Bagasha, Timesmajira Online, Tanga
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Mkoani Tanga wamesema asilimia 23.3 ilioongezwa na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mishahara yao itawapa unafuu kwenye maisha na hivyo kumaliza kilio chao cha muda mrefu.
Akiongea na waandishi wa habari Kwa niaba ya watumishi wa wilaya hiyo Mkuu wa wilaya hiyo Halima Bulembo amesema kuwa wamepata faraja Kwa uamuzi huo na hivyo kuongeza Imani Kwa serikali Yao Kwani kilikuwa ni kilio Chao Cha muda mrefu.
Bulembo amesema wafanyakazi wengi wamepata faraja baada ya tamko la mheshimiwa Rais na wameongeza imani na serikali yao.
Mmoja wa watumishi hao Saumu Mohamed amesema wanamshukuru Rais Kwa ongezeko Hilo kwani watumishi wamefurahi Sana na kumuombea Kwa Mungu aweze kuleta mabadiliko mengi ndani ya nchi hii.
Kwa upande wake Afisa Elimu Selapyone Bashangwe amempongeza Rais Kwa uamuzi wake wa kuongeza mshahara kwani umekuja wakati mwafakaOngezeko la mishahara limekuwa likipigiwa kelele na wafanyakazi kwa muda mrefu hasa wakati wa sherehe za wafanyakazi wakitaka serikali kuongeza kiwango cha mshahara ili kiendane na maisha halisi yaliyopo.
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti