January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC agomea maelezo ya mchakato Miradi ya Maendeleo Iringa

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa makini kuisoma taarifa wakati wa ukaguzi wa miradi ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa

 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa makini kukagua miradi ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa

Moja ya miradi ya kitua cha afya ambayo inaendelea kujengwa katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa miradi ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa akifanya kazi kwa mfano wakati wa ukaguzi wa miradi ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

KAMATI ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa imesema haitaki kusikia maelezo ya mchakato kwenye fedha za miradi ambazo zimetoka serikalini kwa wakati ili kuharakisha kukamilisha miradi kwa haraka na kuanza kutumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya halmashauri ya wilaya ya Iringa,mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa kumekuwa na ucheleweshwaji wa ujenzi wa miradi kutokana na uzembe wa wataalam.

Moyo alisema kuwa fedha ambazo zimeletwa na serikali zinatakiwa zitumike kwa wakati kulinga na majukumu ambayo yanatakiwa kutekelezwa kulingana na thamani ya fedha ambazo zimeletwa kwenye miradi husika.

Alisema kuwa fedha zikiwa zinaletwa kwenye miradi halafu hazitumiki kwenye miradi kwa wakati zitaleta doa kwa halmashauri husika na kushindwa kupewa fedha nyingine kwa ajili ya kutekeleza miradi mingine.

Moyo aliwataka wataalam na wakandarasi kubadilika katika utendaji wao wa kazi ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika jitihada za kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha mkuu wa wilaya Mohamed Moyo alikemea vitendo vya baadhi ya wananchi kuiba vifaa vya ujenzi jambo ambalo linakuwa linarudisha nyuma maendeleo ya ujenzi huo hivyo serikali ya wilaya ya Iringa haitamvumia mtu yeyote atakaye hujumu miradi ya maendeleo.

Moyo alisema kuwa miradi yote inatekelezwa kwa ajili ya kusaidia juu za wananchi katika kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo katika maeneo husika ambako miradi inatekelezwa.

Alisema kuwa miradi yote inatakiwa kutekelezwa usiku na mchana kwa kuwa fedha zipo na zimetolewa kwa wakati kwenye miradi husika na kutekeleza miradi hiyo kwa wakati.

Moyo aliwataka wataalam wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kuendelea kubuni vyanzo v ipya vya mapato ya ndani ambavyo vitasaidia kuchochea maendeleo ya wananchi katika halmashauri husika.

Kwa upande wake kaimu Mhandisi ujenzi halmashauri ya wilaya ya Iringa Eng Nicos Kasililika alisema kuwa wameyapokea maagizo yote ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa na kuahidi kuyafanyia kazi kwenye miradi yote inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.

Eng Kasililika alisema kuwa kamati ya ulinzi na usalama imefanikiwa kutembelea jumla ya miradi mitano inayotekelezwa kwa kutumia fedha kutoka serikali kuu yenye lengo la kuchochea maendeleo kwa wananchi.