January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC aagiza mabucha vingunguti kufunguliwa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija, ameagiza mradi wa machinjio ya Serikali yaliopo Vingunguti Wilayani Ilala ,kufunguliwa AGOSTI mwaka huu .

Mkuu wa Wilaya Ludigija aliyasema hayo katika ziara ya Jimbo la Segerea kukagua Miradi ya Serikali iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli, ambapo katika ziara hiyo walikagua mabucha ya nyama Vingunguti,ujenzi wa Shule ya Sekondari Liwiti na eneo la ujenzi wa Soko la Liwiti.

“Naagiza Mradi huu wa Serikali mabucha haya ya Vingunguti Agosti 10/22 mwaka huu yaanze kazi wafanyanyaniashara waanze kutumia mara moja sitaki kuona kona kona ,pia naagiza mtumie Wakandarasi wenye uwezo katika kuwapa tenda mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Jiji msiwape tenda Wakandarasi wasio na uwezo “alisema Ludigija .

Aidha Mkuu wa Wilaya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji pamoja na Meya wa Halmashauri hiyo kufatilia ujenzi huo kwa karibu kwani ni sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ameagiza Halmashauri hiyo isimamie mapato vizuri katika machinjio ya Vingunguti uchinjaji wake umeshaanza katika machinjio ya Kisasa wote wachinje katika machinjio hayo.

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli ,alipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan katika kuwekeza miradi mikubwa ya Maendeleo Jimbo la Segerea na kukuza uchumi .

Mbunge Bonah Kamoli aliomba Vijana wa Jimbo la Segerea waweze kupata ajira katika MABUCHA ya Nyama na machinjio ya VINGUNGUTI

Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto alisema hatua ya mwisho ya kumalizia ujenzi katika MABUCHA ya Nyama Vingunguti Wilayani Ilala inatarajia kuanza kesho Julai 27/2022 Ili waweze kwenda na agizo lililotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija akitoka kukagua mradi wa mabucha ya Nyama Vingunguti Wilayani Ilala,(Kulia)Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto,Serikali imeagiza mradi huo wa machinjio kufunguliwa AGOSTI Mwaka huu (Na Heri Shaaban )