December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Das.Msengi akabidhiwa ofisi,ahidi maendeleo Ilemela

Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza

Katibu Tawala mpya wa Wilaya ya Ilemela Wakili Mariam Abubakar Msengi amekabidhiwa rasmi ofisi kwa ajili ya kuendelea na shughuli za kuwatumikia wananchi huku akiahidi maendeleo kwa wakazi wa Ilemela.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo, Katibu Tawala Wilaya ya Ilemela Wakili Mariam Abubakar Msengi amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kumuamini na kumteua kwa ajili ya kumsaidia kuwatumikia wananchi wa wilaya hiyo.

Wakili Msengi ameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya Rais Samia ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na maendeleo.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa zamani wa Wilaya ya Ilemela ambaye amehamishiwa Wilaya ya Shinyanga Said Kitinga amewashukuru watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote alichokuwa akifanya kazi pamoja.

Hivyo amewaomba kuendelea na ushirikiano huo kwa Katibu Tawala wa sasa ili aweze kutimiza wajibu wake kwa ufanisi huku akikemea ukwamishaji kwa viongozi.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ilemela Nobert Ndika ambapo amewapongeza viongozi wote wawili kwa kuaminiwa na Rais Mhe huku akiahidi ushirikiano Kwa Katibu Tawala huyo.

Baadhi ya watumishi wa Wilaya ya Ilemela wakiwemo Suzana Tumalinywa na Lightness James wameahidi ushirikiano ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma na kutekeleza shughuli za maendeleo.

Hafla ya makabidhiano ya ofisi kati ya viongozi hao wawili imeshuhudiwa na wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Ilemela katika ofisi za Mkuu wa wilaya hiyo iliyopo Buswelu jijini Mwanza.