*Mkutano utahusisha uchaguzi wa viongozi wa CWT Taifa
Na Mwandishi Wetu Timesmajira Online
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimetangaza kufanyika kwa mkutano mkuu wa chama hicho Mei 28 na 29 mwaka huu, mkoani Dodoma, ambao utahusisha uchaguzi wa viongozi wa kitaifa
Taarifa kutoka ofisi ya Katibu Mkuu wa CWT, Mwalimu Joseph Misalaba, ambaye kwa sasa anakaimu nafasi hiyo imeeleza kuwa mkutano huo wa saba unafanyika baada a chama hicho kukamilisha chaguzi za ngazi za chini ambazo ni ngazi ya shule, ngazi ya wilaya na mkoa ambapo hivi sasa wanaelekea kwenye ngazi ya Taifa.
Taarifa hiyo iliyosasainiwa na Ofisa Habari na Uhusiano wa chama hicho inazitaja nafasi zinazotarajia kuwaniwa ni Rais,Makamu wa Rais,Katibu Mkuu,Naibu Katibu Mkuu na Mweka Hazina.
Nafasi nyingine ni mwakilishi wa walimu wanawake, mwakilishi walimu walemavu, mwakilishi walimu vijana na wadhamini wa chama.
More Stories
Mixx by Yas, UBX, SCCULT kushirikiana kurahisisha huduma za mikopo
TMA yatoa mwelekeo msimu wa kipupwe Juni-Agosti
DC Mpogolo atoa mwezi mmoja pikipiki za umeme zisajiliwe