April 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi wa Itifaki na Mafunzo CUF Taifa, Masoud Omar Mhina akiongea na wanachama wa chama hicho visiwani Pemba juu ya namna chama hicho kilivyodhamiria kuuanika ukweli wa Maalim Seif. Picha na Hadija Bagasha, TimesMajira, Pemba.

CUF yaahidi kuanika ukweli wa Maalim Seif

Na Hadija Bagasha Pemba,

Mkurugenzi wa itifaki na mafunzo CUF Taifa, Masoud Omar Mhina ameahidi kuhakikisha kipindi chote cha kampeni anasotea Zanzibar ili kuanika ukweli wa Maalim Seif Sharif Hamad kuwa siasa za kudanganya watu kwa maslahi binafsi.

Masoud amesema hayo alipongea na wanachama wa chama hicho katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba na kuwa watapita kijiji kwa kijiji, jimbo kwa jimbo kuuanika ukweli wa Maalim Seif.

Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akigawa kadi kwa wanachama wapya zaidi ya 300 wa jimbo la Gando huku wazee wakimlilia marehemu Mwalim Khalifa Suleiman aliyekuwa katibu Mkuu wa chama hicho kwa jimbo hilo ambaye alifariki hivi karibuni. Wazee hao waliangua kilio baada ya kumuona Profesa Lipumba. Picha na Hadija Bagasha, TimesMajira, Pemba

Amesema Wazanzibar wanmini kuwa Maalim Seif anawatetea jambo ambalo si kweli bali yupo kwa maslahi yake. Wazanzibar wanapaswa kuchuja ukweli na uongo na chama kimedhamiria kuuanika ukweli wote wa Maalim kwa Wazanzibar na Wapemba.

”Maalim akija bara anajisifia kuwa Wazanzibar nimewashika hakuna hata mmoja anayepinga, nikiwaambia wote mbele tembea wanakwenda, nyuma geuka wanageuka na nikiwaambia wote kaeni chini watakaa. Ndugu zangu mtayafanya haya miaka yote hadi lini?” Masoud amewahoji wanachama hao.

Ameongeza kuwa, mmejenga chama kwa miaka 27, leo mnakuja kuondolewa na mtu ambaye siyo mkweli kabisa na kama angekuwa mkweli basi mngeona kile anachokisimamia.

”Maalim alisema CUF inashindwa kuingia serikalini kwasababu ndani ya chama kuna wanafki kibao kwaiyo hatutaweza kuingia serikalini mpaka wanafki watoke, sasa mimi nasema namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba wanafki wote wameondoka ndani ya chama hicho akiwemo yeye na wamebaki wakweli watupu,”amesisitiza Masoud.

Mmoja wa wananchama wa CUF, Masoud Hamad Salim amesema jamii inapaswa kuondoa mtazamo wa kwamba chama cha wananchi CUF kimekufa na kwamba kipo imara na kitaendelea kuungwa mkono.

Amesema watahakikisha wanatetea majimbo yote 18 ya Pemba ili waweze kupeperusha bendera ya chama kama ilivyokuwa na wanaamini watapata ushindi kwa kishindo kwani CUF ipo moyoni mwa wananchi.

”Kilichowapoteza watu ni propaganda aliyopiga Maalim kwamba CUF imekufa kitendo ambacho si cha kweli….chama kipo hai na kinaendelea na mapambano, tutaendelea kumuunga mkono Profesa Lipumba ambaye ndio kiongozi tunayemuamini,” amesema mwanachama huyo

Mwananchama mwingine amesema chama hicho kina tamani ushindi wa nguvu na kishindo na wananchi waelewe chama kipo na kitashinda kwasababu ni chama kilichokuwa hakina fujo.

”CUF ni chama cha new model hakuna fujo na kinakwenda kisomi zaidi chini ya Mwenyekiti wake Profesa Ibrahim Lipumba na siyo chama cha kununiana,”amesema mmoja wa wanachama hao.