Na Hadija Bagasha Pemba,
Mkurugenzi wa itifaki na mafunzo CUF Taifa, Masoud Omar Mhina ameahidi kuhakikisha kipindi chote cha kampeni anasotea Zanzibar ili kuanika ukweli wa Maalim Seif Sharif Hamad kuwa siasa za kudanganya watu kwa maslahi binafsi.
Masoud amesema hayo alipongea na wanachama wa chama hicho katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba na kuwa watapita kijiji kwa kijiji, jimbo kwa jimbo kuuanika ukweli wa Maalim Seif.
Amesema Wazanzibar wanmini kuwa Maalim Seif anawatetea jambo ambalo si kweli bali yupo kwa maslahi yake. Wazanzibar wanapaswa kuchuja ukweli na uongo na chama kimedhamiria kuuanika ukweli wote wa Maalim kwa Wazanzibar na Wapemba.
”Maalim akija bara anajisifia kuwa Wazanzibar nimewashika hakuna hata mmoja anayepinga, nikiwaambia wote mbele tembea wanakwenda, nyuma geuka wanageuka na nikiwaambia wote kaeni chini watakaa. Ndugu zangu mtayafanya haya miaka yote hadi lini?” Masoud amewahoji wanachama hao.
Ameongeza kuwa, mmejenga chama kwa miaka 27, leo mnakuja kuondolewa na mtu ambaye siyo mkweli kabisa na kama angekuwa mkweli basi mngeona kile anachokisimamia.
”Maalim alisema CUF inashindwa kuingia serikalini kwasababu ndani ya chama kuna wanafki kibao kwaiyo hatutaweza kuingia serikalini mpaka wanafki watoke, sasa mimi nasema namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba wanafki wote wameondoka ndani ya chama hicho akiwemo yeye na wamebaki wakweli watupu,”amesisitiza Masoud.
Mmoja wa wananchama wa CUF, Masoud Hamad Salim amesema jamii inapaswa kuondoa mtazamo wa kwamba chama cha wananchi CUF kimekufa na kwamba kipo imara na kitaendelea kuungwa mkono.
Amesema watahakikisha wanatetea majimbo yote 18 ya Pemba ili waweze kupeperusha bendera ya chama kama ilivyokuwa na wanaamini watapata ushindi kwa kishindo kwani CUF ipo moyoni mwa wananchi.
”Kilichowapoteza watu ni propaganda aliyopiga Maalim kwamba CUF imekufa kitendo ambacho si cha kweli….chama kipo hai na kinaendelea na mapambano, tutaendelea kumuunga mkono Profesa Lipumba ambaye ndio kiongozi tunayemuamini,” amesema mwanachama huyo
Mwananchama mwingine amesema chama hicho kina tamani ushindi wa nguvu na kishindo na wananchi waelewe chama kipo na kitashinda kwasababu ni chama kilichokuwa hakina fujo.
”CUF ni chama cha new model hakuna fujo na kinakwenda kisomi zaidi chini ya Mwenyekiti wake Profesa Ibrahim Lipumba na siyo chama cha kununiana,”amesema mmoja wa wanachama hao.
More Stories
Serikali yaja na mwarobaini wa changamoto ya Kivuko Magogoni – Kigamboni
Kisarawe kukata keki ya Birthday ya Rais Samia
Wataalam wa afya wakutana kujadili ugonjwa wa Marburg