Na Cresensia Kapinga, Timesmajiraonline, Songea
ZAIDI ya wateja 380,000 wakiwemo watumishi wa Serikali,wafanyabiashara, wanafunzi na wajasiriamali wamejiunga na huduma ya CRDB Al Barakh ambayo inatoa fursa kwa watu kupata huduma kuendana na imani zao hapa nchini.
Akizungumza kwenye hafla ya kufuturisha wateja na wadau wa benki hiyo iliyofanyika jana mkoani Ruvuma jana, Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki hiyo, Mussa Kitambi alisema huduma za Al Barakh zimefuata misingi ya sheria.

Amesema huduma hizo zinapatikana katika matawi yote nchini mpaka sasa wameweza kutoa uwezeshwaji wa zaidi ya sh. bilioni 172 na kwamba wanajivunia ubunifu huo ambao umekuwa na mwitikio mkubwa wa wateja.
“Tunapoendelea na funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ninawiwa kukawakaribisha kuendelea kutumia huduma zetu za Al Barakh zinazofuata misingi ya sheria.
Wateja wetu wanaweza kutunza amana zao na kufanya miamala kupitia akaunti maalumu za Al Barakh iwe ni kwa wanafunzi,wafanyakazi, wafanyabiashara au wajasiliamali ambapo wanaunganishwa na kadi maalumu za Al Barakh. ” alisema Kitambi.
Awali akizungumza kwenye hafla hiyo meneja wa CRDB Kanda ya Kusini, Denis Mwoleka, alisema kuwa benki ya CRDB imekuwa na utaratibu na utamaduni wa kuandaa futari kwa ajili ya wateja na wadau wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani wakiamini kuwa funga ya Ramadhani ni shule ya mafunzo ya maadili mema, upendo na mshikamano.
“Napenda nichukuwe fursa hii kuwashukuru sana kwa sapoti mnayotupatia benki yetu ya CRDB kupitia dirisha letu tunaloliita Al Barakh benki kwa kweli tunashukuru sana tumefungua akaunti nyingi lakini tumefanya biashara nyingi kupitia biashara yetu ya Al Barakh na naamini kabisa kwamba tunapoenda kuanza kujiandaa na imani hii basi mnafahamu kuwa kuna dirisha zuri ambalo lipo ndani ya CRDB linalowawezesha kufanya huduma ” alisema Mwoleka .
Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa, Ramadhani Mwakilima, amesema kuwa dirisha hilo la Al Barakh limesimamiwa kwa ukamalifu na Baraza Kuu la Uisilamu la Tanzania BAKWATA chini ya Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi na ukienda kwenye Ofisi ya Sheikh wa Mkoa yeyote Tanzania utakuta kuna walaka Maalum unaomtaka huyo Sheikh kuhakikisha anasimama na kuisimamia Al Barakh katika Mkoa wake.

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Kapenjama Ndile ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas amesema utaaratibu wa benki ya CRDB wa kuandaa futari hiyo maalumu kwa wateja na wadau wao katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ni jambo jema kwani linaleta mshikamano baina ya wateja na watumishi wa benki hiyo.

More Stories
The Desk and Chair yatoa vifaa saidizi kwa Masatu na mkewe
jengo la mama,mtoto la bilioni 6.5 lazinduliwa Mbulu
Dkt.Malasusa ataka hospitali ya Haydom kuombea wafadhili wanaoishika mkono