January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CPA Makalla: Nguvu ya CCM inatokana na Mabalozi, Viongozi wa Shina na Mitaa

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar

KATIBU wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla, ameanza ziara yake ya kichama ya siku tatu katika Mkoa wa Dar es salaam, huku akisisitiza kuwa nguvu kubwa ya CCM inatokana na Mabalozi,  Viongozi wa Mashina na Mitaa.

CPA Makalla amesema hayo leo Agosti 27, 2024 mara baada ya kuzindua Shina la Wakereketwa la Wavuvi Beach, lililopo eneo la Mjimwema katika Wilaya ya Kigamboni lililoanzishwa Juni 24 mwaka huu, lenye Wanachama zaidi ya 150, ambapo pia amewapatia Shilingi Milioni moj ili iwasaidie katika kuendeleza shina hilo.

Aidha, CPA Makalla, ameutaka uongozi na wanachama wa shina hilo kufanya kazi kwa niaba ya CCM katika eneo hilo kwa niaba kwa kueneza sera, ushawishi kwa watu na kueleza Utekelezaji wa Ilani ya CCM na kusema hayo ndio yawe majukumu yao Katika shina hilo.

Pia, CPA Makalla, amesema shina hilo limefunguliwa muda muafaka, hivyo kazi yake kubwa ni kuhakikisha CCM inashinda Uchaguzi wa Serikali za mitaa.

“Naomba viongozi, Wanachama na wadau wa shina hili kazi yenu kubwa iwe ni kukiombea kura chama chetu na kukisemea Yale yote mazuri kinachofanya” amesema Makalla.

Hata hivyo, ameyataka makundi mengine kuiga mfano wa Wanachama wa shina hilo, kwa kujishughulisha katika shughuli mbalimbali za kujipatia kipato.