Na Mwandishi wetu, Timesmajira
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitatumia 4R za Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kampeni za kistaarabu na kuheshimiana katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.
Amesisitiza kuwa viongozi na wanachama wa CCM watakaopata fursa ya kuzungumza katika majukwaa ya kisiasa katika kampeni za uchaguzi huo, watajikita kueleza maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Rais Dk. Samia katika ngazi ya vijiji, vitongoji na mitaa.
Makalla aliyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, wakati akizungumza na maelfu ya wanachama na viongozi wa CCM Wilaya ya Ilala kwenye ukumbi wa Mwigo Tabata,ambapo alitumia fursa hiyo kuelelezea msimamo wa CCM kuelekea uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
“Uchaguzi huu utaongozwa na 4R za Mheshimiwa Rais ambazo ni Maridhiano (Reconciliation), Ustahamilivu (Resilience), Mageuzi (Reforms), na Kujenga upya Taifa (Rebuilding). CCM inaahidi kufanya kampeni za kistaarabu, hivyo tunaviomba vyama vingine pindi ambapo kampeni zitakapoanza, twendeni na 4R.
“Tujenge hoja na tutofautiane kwa itikadi kwani tuna Tanzania moja. Uchaguzi uiache Tanzania ikiwa moja yenye amani na utulivu. CCM tunavyosema ndiyo tunamaanisha,”amesema
Makalla amesisitiza kuwa mambo yaliyofanywa na Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kila mwanaCCM akipewa nafasi ya kuongea jukwaani ataongea mambo mengi yaliyofanywa. Kwa hiyo kwetu sisi matusi, kejeli haitokuwa sehemu yetu.”
More Stories
CCM kutumia 4R za Samia Uchaguzi Serikali za Mitaa
Dkt. Mpango awasilisha salam za Rais Samia mazisha Baba yake mzazi, Gavana Tutuba
5 “best” Bitcoin Online slots games