Na Irene Fundi, timesmajira
MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ametambulisha rasmi kongamano la taifa la maonesho ya Sayansi,technolojia na ubunifu litakalotarajia kufanyika June 14 na 15,Mwaka huu.
Akizungumza leo na waandishi wa habari kuelekea kongamano hilo amesema kuwa kongamano hilo ni mkakati wa tume katika kutekeleza jukumu lake la msingi la kuhabarisha umma kuhusiana na kazi zinazoendelea nchini.
Nungu amesema katika kongamano hilo ambalo linakaulimbiu lisemalo “Sayansi na Ubunifu Kwa Maendeleo Endelevu”ambapo lengo la kongamano hilo ni kuwezesha watafiti, wabunifu,wanasayansi na watunga Sera kukutana pamoja ili kujadili,kubadilishana mawazo na kupeana taarifa mbalimbali kuhusu masuala ya teknolojia na ubunifu nchini.
Pia amesema kuwa wabunifu na wavumbuzi watapata fursa ya kusikiliza kutoka katika serikali na wizara zake mbalimbali zinamipango ipi ambayo wao wanaweza kuendana nayo na endapo changamoto yoyote itatokea watafuata miongozo itakayo kuwepo.
Amesema katika kongamano hilo kutakuwepo na mada mbalimbali ikiwemo Mapinduzi ya viwanda, sayansi na ubunifu wa uchumi wa kijani,mchango wa maaarifa asilia na sayansi huria.
Nungu amesema kuwa Ubunifu upo mwingi lakini wabunifu wanatakiwa kuwa na ubunifu unaoangalia mbele zaidi na wenye kuleta maendeleo Tanzania.
Pia amesema kuwa kongamano hilo litahudhuliwa na Watafiti,wabunifu, wanasayansi na wafanya maamuzi ili kujadili na kutoa mawazo mbalimbali kuhusu wizara ya Sayansi na Teknolojia.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi