Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online,Morogoro
MENEJIMENTI ya Chuo Kikuu Mzumbe imeutambulisha mradi wa mageuzi ya sekta ya elimu kwa ajili ya kuchochea uchumi ‘Higher Education for Economic Transformation – HEET’ wenye lengo la kuongeza udahili kwa kujenga miundombinu na kuboresha mitaala ili kuendana na soko la ajira la sasa.
Akizungumza katika kikao na Wafanyakazi wa Kampas kuu Morogoro, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof.Lughano Kusiluka, amesema ni vyema Watumishi kujiandaa na kuchangamkia fursa zilizopo katika mradi huo mkubwa wa miaka mitano ambao utahusisha ujenzi wa miundombinu na kuwaendeleza Watumishi kitaaluma.
“Ifikapo mwaka 2025 majengo yanapaswa kuonekana na hivyo tunapaswa kuwa na kasi kubwa ya utekelezaji wa mradi huo” amesisitiza Prof.Kusiluka.
Awali akitoa taarifa kuhusu mradi huo Mratibu msaidizi wa mradi huo,Dkt.Hawa Tundui, amesema Chuo kikuu Mzumbe kimetengewa Dola Milioni 22, kwa ajili ya kutekeleza mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, ambapo asilimia 80 ya fedha hizo ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na 20 ni kwa ajili kuwaendeleza Watumishi kitaaluma na kutengeneza mitaala mipya ya elimu.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa