November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chuo cha anga kutoa kozi ya ‘drone’


Na Joyce Kasiki Dodoma

CHUO cha Usafiri wa Anga (CATC), kimewaasa wananchi kujiunga na chuo cha urushaji ndege nyuki (drone) na hivyo kuwezesha watu wengi kujua kuitumia Teknolojia hiyo na kuleta tija katika sekta ya kilimo nchini

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la CATC kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma ,
Ofisa Habari na Masoko Mkuu wa Chuo hicho, Ally Changwila amesema,chuo hicho kimeanzisha kozi hiyo ili kusaidia wakulima hasa katika unyunyiziaji wa dawa mashambani na kutambua visumbufu vya mazao kama nimeingia shambani.

‘Kwa hiyo tumekuja katika maonesho haya, ili kuwafahamisha wananchi kuhusu chuo chetu ambacho kinatoa kozi ya urbano wa ndege nyuki inayowahusu wakulima moja kwa moja.

Aidha amesema kozi hiyo inatolewa kwa wiki nne, ambapo wiki mbili mwanafunzi atasoma darasani na wiki mbili kwa vitendo na muhusika anakuwa ameiva tayari kwa kupata leseni ili aweze kufanya kazi.

“Kwa sasa mtu akirusha ndege nyuki bila kuwa na leseni inayotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ataingia katika matatizo.”amesema

Amesema kozi hiyo pia itamsaidia mkulima au muhusika aliyejifunza kozi hiyo ,kumwagilia dawa kwenye mazao na kufanya ukaguzi ili kujua maeneo ambayo mazao yanavamiwa na wadudu na kufanya ufuatiliaji kabla ya madhara makubwa kutokea.