LOS ANGELES, California
NYOTA wa muziki nchini Marekani, Chris Brown amelipotiwa kuwa chini ya Uangalizi wa polisi baada ya kudaiwa kumpiga mwanamke mmoja wikiendi hii baada ya wawili hao kugombana.
Kwa mujibu wa Mtandao wa TMZ Umesema, msanii huyo amedaiwa kumpiga mwanamke huyo kichwani kiasi cha kumtoa nywele zake baada ya kutokea ugomvi kati yao.
Polisi wamedai wamepata ushahidi kutoka kwa msanii San Fernando ambaye alikuwepo kwenye nyumba hiyo wakati tukio hilo linatokea wikiendi hii.
Mwanamke huyo ameviambia vyombo vya sheria kuwa ameumizwa maeneo ya kichwani na msanii huyo ambaye kwa muda sasa amekuwa kwenye matatizo mara kazaa na wanawake.
Chris brown amewahi kuingia kwenye kesi nzito ya unyanyasaji wanawake baada ya kumpiga msanii mwenzake, Rihanna ambaye kwa wakati huo alikuwa mpenzi wake.
Hata hivyo, Polisi wamedai mwanamke huyo hajaumizwa kama inavyodaiwa na wanaendelea na uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA